27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Waziri aagiza ukarabati wa chuo kukamilika kabla ya mwaka kuisha

Asha Bani-Dar es Salaam

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameuagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(CKD), kuhakikisha wanakamilisha ukarabati wa chuo hicho kabla ya kufunguliwa Novemba mwaka huu.

Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam wakati wa ukaguzi wa maendeleo  ya miradi  ya ukarabati wa bweni, majengo ya Ndaki ya uhandisi na Teknolojia (CoET)na ukarabati wa mfumo kusambaza maji safi na salama.

Profesa Ndalichako ameridhishwa na ukarabati wa majengo hayo lakini amesisitiza ukamilike kabla wanafunzi kufungua chuo ili waweze kufikia katika majengo mazuri na huduma nzuri inayokidhi kiwango cha elimu bora.

Naye Makamu Mkuu wa chuo hicho profesa William Anangisye amemuhakikishia Waziri Ndalichako kutekeleza agizo lake na kwamba wahandisi wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kazi hiyo inakwisha kwa kiwango cha hali ya juu.

“Mabweni yaliyokarabatiwa yatachukua wanafunzi 778, ukarabati milango 10 kati ya 400 imeshapachikwa na mingine tayari imetengenezwa kwa sasa hali ni nzuri na ukarabati umekamilika kwa asilimia 80,”amesema Anangisye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles