27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

WAZIRI AAGIZA OFISA USTAWI KUHUDUMIA WAZEE HOSPITALI

Na BENJAMIN MASESE

SERIKALI imeagiza  uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza SekouToure kuhakikisha ofisa ustawi anakuwapo  kwenye dirisha  la matibabu kwa wazee   kuwaondolea usumbufu kwa kupata vibali vya kuhudumiwa bure.

Agizo hilo lilitolewa juzi na Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile  alipotembelea  hospitali hiyo    kujionea jinsi huduma zinavyotolewa na kuzungumza na wagonjwa.

Dk. Ndugulile alisema pamoja na kuridhishwa na jinsi huduma zinavyotolewa katika hospitali hiyo  ni lazima   uwepo   utaratibu mzuri kwa ofisa ustawi wa jamii  apatikane maeneo ya huduma kwa ajili ya kutoa vibali vya huduma bure kwa wazee.

“Muweke utaratibu kuhakikisha wazee wanaokuja hawazunguki huku na kule kumtafuta ofisa ustawi wa jamii kwa ajili ya kuwaandikia vibali vya huduma bure.

“Hakikisheni  anakuwapo hapa hapa  wazee wasikae muda mrefu hospitalini na wapate huduma staiki,” alisema Ndugulile.

Mganga Mkuu wa Mkoa Dk.Rutachunzibwa Thomas, alimweleza waziri   kwamaba  kuongezeka kwa vituo vya afya vyenye nyota tatu kutoka  kimoja mwaka 2015 hadi vituo 116 mwaka huu ni ushahidi wa kuimarika kwa sekta ya afya.

“Huduma imeimarishwa kwa sababu hata wiki iliyopita tulikuwa na  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu  amezindua Mpango wa Kuboresha Afya ya Uzazi kwa Wajawazito na Watoto (IMPACT) unaotekelezwa na Aga Khan Development, Network kwa ufadhili wa serikali ya Canada utakaogharimu Sh  bilioni 25.

“Mpango huu unatekelezwa katika  halmashauri zote nane za wilaya saba    mkoani Mwanza… hii kwetu ni mafanikio makubwa,” alisema Dkt. Thomas.

Dk.Thomas alisema  serikali  imewezesha  kupata  asilimia 96 hadi 98 ya fedha ya dawa na vifaa tiba wakati awali walikuwa wakipata  asilimia  46  tu.

Alisema  ongezeko hilo  limefanikisha   kuboreha huduma ya afya huku akimkumbushia  ahadi ya Mashine ya Mionzi (CT SCAN ) iliyoahidiwa  na Waziri Ummy Mwalimu.

Alisema   mpaka sasa  chumba maalumu kwa ajili ya mashine hiyo kimeandaliwa kama alivyoagizwa na Serikali hivyo kinachosubiriwa ni mashine hiyo.

Dk. Ndugulile pia  aliziagiza hospitali zote nchini kuepuka kuwaandikia wagonjwa dawa ambazo hazipatikani maeneo ya huduma  kuepukana na usumbufu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,327FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles