25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri aagiza mradi wa maji Chalinze kupitiwa upya

Tunu Nassor-Dar es Salaam

Wizara ya Maji inatarajia kuunda tume maalumu itakayopitia upya mradi wa maji wa Chalinze Mboga baada ya kuukuta na mapungufu mengi katika utekelezaji wake.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kutembelea mradi huo na kubaini udanganyifu wa vipimo vya ulazaji mabomba.

Akitoa maamuzi hayo, Mbarawa amesema mkandarasi kampuni ya Shanx wamefanya udanganyifu wa vipimo vya ulazaji wa bomba pamoja na kutaka nyongeza ya gharama ya mradi kulingana na kiwango cha mawe alichokuta kwenye eneo la mradi.

Mbarawa amesema, amefikia maamuzi ya kuunda tume maalaum ili kuweza kupitia upya mradi huo ikiwemo na kuwaita Dawasa na Shanx ofini kwake ili kupitia upya  maombi ya mkandarasi huyo.

“Ntawaita ofisini kwangu Dawasa pamoja na Mkandarasi ili kuweza kupitia maombi yao juu ya ongezeko la gharama za uchimbaji na ulazaji bomba, pia ntaunda tume maalumu itakayopitia upya mradi wa Chalinze Mboga,” amesema Mbarawa.

Amesema, makubaliano ya awali ni kuchimba mtaro wa kulaza mabomba mita 1.8 ila wao wamechimba mita 1.6 kwenda chini tofauti na makubaliano yaliopo kwenye mkataba.

“Katika mkataba makubaliano ilikuwa kuchimba mita 1.8 kwenda chini na wanalipwa kulingana na kipimo cha uchimbaji ila kulingana na wanavyochimba ina maana malipo yao sio sahihi,” amesema 

Ameeleza kuwa mkandarasi wa mradi huo gharama zake za uchimbaji zipo juu ambapo anapima mita 1 kwa shilingi 49,000 wakati Arusha ni shilingi 32,000 kwa mita na wanachimba mita 2 kwenda chini. 

Mbarawa ameendelea na kusema kuwa, mkandarasi ameandika maombi ya ongezeko la gharama za uchimbaji na ulazaji bomba kulingana na kiwango cha mawe alichokuta kwenye eneo la mradi.

“Mkandarasi ameandika maombi ya ongezeko la gharama ya uchimbaji na ulazaji wa mabomba kutokana na kiwango cha mawe alichokikuta, jambo haliwezekani kwani atuwezi kuingiza pesa ya serikali kwa namna hii kilichobaki ni kuwatafuta wataalam ili waupitie pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles