28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Waziri aagiza mkandarasi kuwekwa ndani

Derick Milton, Maswa

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, ameagiza kukamatwa ndani kwa Mkandarasi wa Kampuni ya ukandarasi PET CO Operation, inayojenga mradi wa chujio la Maswa katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Tryphone Elias, kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo kwa wakati.

Mradi huo unaogharimu kiasi cha Sh bilioni 3.5, ambapo ulitakiwa kujengwa kwa muda wa miezi minane lakini umetimiza miaka minne tangu mwaka 2015 bila ya kukamilika ujezi wake.

Jana usiku Waziri huyo alifanya ziara ya ghafla kukagua ujenzi unavyoendelea kabla ya kutoa maagizo hayo Waziri huyo alisema kuwa mkadarasi huyo amepewa miradi 15 kwenye maeneo mbalimbali nchini, ambayo yote imeshindwa kukamilika kwa wakati.

“Pale Wizarani ulitumia njia za rushwa ukapewa hii miradi, haiwezekani miradi yote 15 mtu mmoja na yote imemshinda, hakuna mradi ambao umekamilisha ujenzi wake, umeendelea kukatili wakazi wa Mji wa Maswa kutumia maji yenye tope,” amesema Waziri Mbarawa.

Baada ya kusema hayo, aliwatakab Kamanda wa Polisi Wilaya ya Maswa na Mkuu wa Wilaya kusimamia Mkandarasi huyi akamatwe na kuwekwa ndani kwa saa mbili na muda huo ukiisha aandike maelezo ndani ya siku 11 awe amekamilisha akishindwa kuandika hayo maelezo vizuri asitoke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles