Waziri aagiza kuundwa tume ya uchunguzi fedha za ujenzi

0
516

Amina Omari, Muheza

Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jaffo amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela kuunda tume ndani ya wiki mbili  ambayo itachunguza matumizi ya fedha katika ujenzi wa mradi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza.

Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri huyo kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huku ikiwa zaidi ya asilimia 80 ya fedha zikiwa zimetumika.

Ameyasema hayo leo baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo ilitakiwa kukamilika Agosti 30 mwaka huu.

“Kwakweli Muheza sijaridhishwa na kasi ya ujenzi hivyo natoa mpaka oktoba 15 majengo haya yawe yamekamilika, bila hivyo nitazuia nyongeza ya fedha nyingine kwa ajili ya kumaliza miundombinu mingine katika hospitali hii” amesema Waziri Jaffo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here