WAZEE WAKUMBUKWA ZANZIBAR

0
747
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Kusaidia Wazee, Smart Daniel
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Kusaidia Wazee, Smart Daniel

Na MWAJUMA JUMA-ZANZIBAR

MABADILIKO ya kweli katika mifumo ya kanuni na sheria yatategemea kwa kiasi gani wazee wataweza kuyachukulia kuhakikisha inawapeleka wanapotaka, imeelezwa.

Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Kusaidia Wazee, Smart Daniel aliyaeleza hayo katika mafunzo ya siku tatu ya wazee kuhusu pensheni ya jamii, hali stahiki na namna ya kuzifikia programu na huduma za hifadhi ya jamii kwa wazee.

Alisema hatua hiyo itafikiwa iwapo   taarifa hizo zitatumiwa kwa kushirikiana kwa karibu kati ya wazee hao na Serikali.

Hata hivyo, alisema  Zanzibar imekuwa nchi ya mfano katika suala zima la  kuwahifadhi wazee ikiwa ni pamoja na kuwapatia pensheni kila   mwisho wa mwezi.

Alisema ingawa kiasi hicho ni kidogo,  nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikiiga kupitia kwao.

“Jambo la  msingi ni kujipanga na kuona kwa kiasi gani wazee hao wanakuwa na ushirikiano na Serikali  kuona penye kasoro panarekebishwa,”  alisema.

Hata hivyo alisema   Serikali kuu imekuwa ikijitahidi lakini changamoto ipo kwa ngazi za chini.

Alisema ni jukumu la wazee kuona  kila jambo ambalo wanataka wakae na kushauriana na baadaye taarifa ziweze kufikisha kunakohusika kinyume chake hawataweza kufikia malengo.

Alisema shirika lao limeamua kufanya Tanzania kuwa mwenyeji wa mouton   Novemba ikiwa na lengo la  kusherehekea nchi ndogo kama Zanzibar kufanya jambo kubwa kwa wazee wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here