24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wazee Simba kuvamia kambi ya wachezaji

Pg 32MWALI IBRAHIM NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
BAADA ya Simba kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City juzi, wazee wa klabu hiyo wameshindwa kuvumilia na kuamua kupanga kutinga kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Ndege Beach Dar es Salaam, ili kuzungumza na wachezaji kujua tatizo linalosababisha kuvurunda katika ligi.
Simba msimu huu imeshindwa kufanya vema katika mechi zake mbalimbali za ligi, ambapo kwa sasa inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo hali ambayo imewakasirisha kwa kiasi kikubwa mashabiki wao, huku wengine wakisusia kushuhudia mechi nyingine za timu hiyo.
Habari za kuaminika zilizolifikia MTANZANIA zimedai kuwa, wazee wa klabu hiyo wameamua kuchukua uamuzi huo ili kujua tatizo linaloifanya timu hiyo kushindwa kufanya vema kwenye mechi zao za ligi, hali inayotishia kushuka daraja kama hawatafanya vema.
“Wazee wamekutana leo (jana) na kuamua kuchukua uamuzi huo kuongea na wachezaji na kuwasikiliza matatizo yao, kwani hakuna hata mmoja anayevutiwa na hali ya matokeo ya klabu kwa sasa hivyo wanaimani wakizungumza na wachezaji labda watagundua tatizo na baada ya kutoka hapo watakaa kujadili namna ya kuinusuru timu yao,” alisema.
Wakati huo huo Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, amesema kukosekana kwa kiungo wake mahiri, Said Ndemla, kumechangia timu hiyo kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam juzi.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kopunovic alisema mchezaji huyo ndiye muhimili mkubwa katika timu hiyo kwa sasa, kwani amekuwa akionyesha kipaji cha hali ya juu anapokuwa uwanjani.
Alisema Ndemla ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na anahitaji uangalizi mzuri ili kuisaidia timu hiyo na taifa kwa ujumla, kwani tangu alipochukua majukumu ya kukinoa kikosi hicho, amekuwa akifurahishwa na juhudi zake.
“Siwezi kumlaumu mchezaji yeyote kwa matokeo ambayo tumepata, mabeki wangu walizembea na baada ya sare ya 1-1, wachezaji wote walichanganyiwa kabisa na kushindwa kuonyesha kiwango kizuri.
“Nitaendelea kumsifia Ndemla, sijawahi kuona mchezaji kama huyu, kwa mara ya kwanza niliona kipaji chake kule Zanzibar nilivutiwa naye sana, tangu nimeanza kazi yangu hakuna kiungo mwenye uwezo kama huyu kijana,” alisema Kopunovic.
Kocha huyo alieleza timu hiyo inaundwa na wachezaji wengi vijana, bado inahitaji muda zaidi kuendelea kujengwa taratibu na kufikia ngazi za juu.
Ndemla ambaye anaendelea kuuguza majeraha ya nyama za paja, amepewa mapumziko ya wiki mbili, baada ya kuumia katika fainali za Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.
Simba kwa sasa imeonekana kuwa na mgawanyiko ambapo mashabiki wamekuwa wakiulalamikia uongozi kuwa ndio chanzo cha timu hiyo kufungwa, kutokana na kutokuwa karibu na wanachama wao kwa pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles