24.1 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

WAZAZI WAWAACHISHA WATOTO SHULE, WAUZA MALI ILI WATALII

 

 

JOSEPH HIZA Na MASHIRIKA,

FAMILIA moja nchini Uingereza imeuza kila kitu ili iishi kwa safari za kuizunguka dunia kwa maisha yao.

Lakini pia iwapo watapata eneo ugenini, ambalo watalipenda mno wataamua kutengeneza makazi ya kuduni.

Wenzi hao, Clare Fisher (31) na mumewe Ian (28), kutoka Porthcawl, Wales kwa sasa wanawaondoa watoto wao wawili kutoka shule ili wasafiri nao katika ziara hiyo ndefu.

Wenzi hao wamezionya familia na marafiki zao kwamba huenda wasirudi tena wakiwa hai nchini Uingereza kwa sababu ‘maisha ni mafupi mno.’

Ili kugharimia safari yao itakayokula fedha nyingi, Clare na Ian wanauza kila kitu kuanza gari lao hadi mabegi ya mikononi ili kuanza upya maisha ya kuizunguka sayari hii.

Clare mama wa binti Maddison (3) na mwana Kallan (5) anasema: “Baada ya kifo cha mwanafamilia na rafiki wa karibu tulikaa kitako siku moja na kuambiana kwanini tusiifanye hii?

“Kama familia tumesafiri mno, wakati mwingine mara tatu kwa mwaka na hivi karibuni ndio tumerufi kutoka Dubai.

“Huwa tunafurahia zaidi iwapo tunasafiri au kupanga kusafiri. Hakuna ukomo wa kiasi cha muda tutakaotumia safarini. 

“Tumepanga safari ya kwanza ya miezi minane na kisha tutarudi kuziona familia na marafiki zetu kabla ya kuendelea na awamu ya pili ya safari,” anasema.

Anaongeza: “Ningependa kufanya safari ya dunia nzima na hatuna mpango halisi wa kurudi. Uwezekano mkubwa ni kutulizana sehemu moja ya moja ya mataifa tutakayotembelea baada ya kuvutiwa nayo zaidi.”

Clare, ambaye ni mtaalamu wa biashara na Ian, ambaye anafanya kazi katika kampuni ya habari, wanaweka akiba kila senti wanayopata na wameshaanza kuuza vitu vyao ili kupata fedha kwa kadiri inavyowezekana.

Lakini iwapo fedha zitaisha wakati wa safari, watatafuta ajira ya muda. Wenzi hao wanawekeza fedha kununua video na kamera kwa ajili ya kuangazia safari yao na kushea simulizi katika akaunti zao za YouTube, Instagram na Facebook.

“Kwa sasa nafanya kazi kutokea nyumbani na hivyo ndivyo nitakavyofanya pia nikiwa ugenini na tunaweza kutumia simulizi zetu kupata fedha pia,' alisema Clare.

“Na daima imekuwa ndoto yetu kujitolea hasa kwa watoto na tunataka watoto wetu wajifunze mapema kuhusu kusaidia wengine,” anasema.

Clare anasema kwamba pia watatumia muda wao safarini kuwasomesha watoto wao kila siku na wanatarajia kufuata mtaala na kusoma kwa njia ya mtandao.

Baada ya kuuza kila kitu walicho nacho wataondoka katika makazi yao wakati wa Christmas na baada ya kutumia siku za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya wataondoka kuanza safari hiyo.

Awamu ya kwanza ya safari yao itawafikisha katika kisiwa cha Majorca, Thailand, Vietnam, Cambodia, Malaysia, the Philippines, Indonesia, Sri Lanka, New Zealand, Australia na Fiji.

Baada ya hapo watarudi nyumbani kabla ya kuelekea Marekani na Canada.

“Wakati tulipoiambia familia yetu na marafiki zetu kuhusu safari hii, siwezi kusema kama walifurahi lakini najua wanatufurahia na watatukosa sana, Clare anasema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,644FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles