29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wazazi watakiwa kutilia mkazo malezi kudhibiti uhalifu

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Imeelezwa kuwa matukio mengi ya uhalifu kwa sasa yamekuwa yakifanywa na Watoto wenye umri chini ya miaka 20 jambo ambalo linaashiria kuwa wazazi na walezi kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Hayo yamebainishwa Juni 16, 2021jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Chanika Mratibu Mwandamizi, Joseph Mwakabonga, wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanywa na Taasisi inayojihusisha na malezi ya watoto waliohatarini kupoteza malezi ya wazazi SOS ambapo amesema ni muhimu kwa wazazi kutekeleza wajibu wao.

“Kila mzazi anatakiwa ashiriki katika malezi ya watoto ili kusaidia watoto wetu kuwa na malezi mazuri yatakayowasaidia kuwa na tabia njema kuepukana na uhalifu unaofanya na baadhi ya watoto.

“Watoto walifanya maandamano ya kudai haki na makaburu waliwauwa na kusababusha vifo vya watoto 1,000 ndio sababu ya kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika.

Aidha, aliongeza kuwa; “Mzazi unatakiwa kujua wajibu wako kwa familia na jamii ili kumsaidia mtoto kuweza kufikia malengo yake na kuachana na uhalifu katika jamii.

Mwakabonga amesema kuwa Jeshi hilo limekuwa likikabiliana na uhalifu unaofanywa na watoto kwenye mitaa mbalimbali hivyo amewataka jamii kushirikiana na Taasisi za malezi katika kula watoto kwenye maadili kwa kuwapatia mahitajika muhimu ikiwemo elimu na makazi salama.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa mradi kutoka SOS, Celestino Mwalongo, amesema maadhimisho hata atumie kama najua ya kuwakumbusha wazazi na walezi kutekeleza majukumu yao

Naye, Mshololo Ondit, kutoka Taasisi ya Mazingira Forum CC aliposhiriki maadhimisho hayo amezungumzia umuhimu wa utunzaji mazingira ili watoto walelewe kwenye mazingira safi na salama.

“Mtoto ndio barua ya kwanza kwenye jamii katika usafi, yeye ndio chanzo na hamasa kwa wazazi na malezi kwenye usafi kuanzia wa shuleni hadi nyumbani,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,220FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles