33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi wasisitizwa kuendeleza vipaji vya watoto

Na Sheila Katikula, Mwanza

Wazazi  na walezi katika kata ya Nyamagana iliyopo jijini Mwanza wametakiwa kutambua vipaji vya watoto wao ili waweze kuwaendeleza  katika masomo na kutimiza ndoto zao za baadae.

Hayo yalisemwa  na Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bhiku Kotecha  kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Nyamagana iliyopo jijini hapa ya kuwapongeza walimu kwa matokeo mazuri.

 Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bhiku Kotecha, akizungumza na waalimu na wadau wa elimu kata ya Nyamagana wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule ya Msingi Nyamagana kwa kutoa mwanafunzi bora katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba.

Alisema kuwa lengo la  hafla hiyo ni kuwapongeza walimu hao kwa juhudi zao za kuimarisha ufaulu kwa wanafunzi wanaohitimu darasa la Saba mwaka jana.

Kotecha alisema kuwa matokeo mazuri kwa Wanafunzi hutokana na kufanya kazi  kwa  ushirikiano kati ya walimu na wanafunzi na kujituma.
Aliongeza pia nidhamu nzuri katika maeneo ya kazi ni njia moja wapo ya kuleta Chachu ya maendeleo ya kielimu katika shule husika. 

Nimefura hishwa na juhudi zenu katika kazi kwani kutoa mwanafunzi  bora wa kwanza siyo mchezo ndiyo manaa nimeatoa  mifuko miwili ya sukari yenye ujazo wa Kl 25, jiko la gesi na ngao  katika shule ya msingi nyamagana kama zawadi ya kuwapongeza walimu,” alisema Kotecha.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Nyamagana, Anadoreen Rugaimukamu alisema kuwa kati ya shule zilizopo kwenye kata 18  wilayani Nyamagana kata ya Nyamagana imekuwa ya kwanza imetoa mwanafunzi bora wa kwanza wa kiume wilayani humo.

Alisema ushindi huo umetokana na ushirikiano  mzuri waliokuwa nao kati ya walimu na wazazi katika suala zima la kutambua umuhimu wa masomo pamoja na  malezi bora.

Jelly Geogre ni Mwanafunzi aliehitimu darasa la Saba katika Shule ya Msingi Nyamagana mwaka 2020  na alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika ngazi ya Wilaya.

Alisema siri ya mafanikio  ni kuwisikiliza walimu kwa umakini walichofundisha na  kujisomea  kwa bidii  ndiyo imepelekea kufanya vizuri kwenye mtihani huo.

“Niliweka utaratibu wa kujisomea mara kwa mara na mwalimu akinifundisha sijaelewa namfata kwa muda wangu ofisini  ili  anielekeze tena, malengo yangu ni kuwa Daktari wa moyo kwa sasa nasoma shule ya sekondari  Ipwaga iliyopo Misungwi jijini hapa,” alisema George.

Kwa upande wake Baba Mzazi wa Jelly alisema kuwa nidhamu nzuri waliyomfunza tangu akiwa mdogo imesaidia kwa kiasi kikubwa kufanya vizuri kwenye  masomo yake.

Afisa Elimu kata ya Nyamagana, Bertha Ntanwa, amewataka walimu  kuendelea na utaratibu waliokuwa wakifanya katika kuwatambua wanafunzi wenye vipaji na kuwaendeleza sanjari na kuwahiza Wenye uwezo mudogo kujituma.

 “Tumetoa vyeti  kama zawadi kwa walimu waliofaulisha vizuri kwenye masomo wanayofundisha nawaomba muendelee kujituma katika kazi ili mwakani tupate watoto wengi waliofanya vizuri,”alisema Ntanwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles