29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wazazi wasiokaa na watoto wao watahadharishwa

Na Sheila Katikula, Mwanza

Mchungaji wa Kanisa la EAGT-Kiloleli lililopo mtaa wa Kiloleli wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Jacob Mtashi amewatahadharisha wazazi wenye tabia ya kutokaa na watoto wao na kupenda kumwachia dada wa kazi kuacha ama kupunguza tabia hiyo kwani imekuwa chanzo cha watoto kubadilika kitabia.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Jacob Mtashi amesema kwa siku za hivi karibuni tabia ya wazazi kutokaa na watoto imekuwa kubwa hali ambayo inayofanya tabia na makuzi ya watoto wengi kutokuwa ya kidini na kiimani na wengi wao kuishia kwenye mfumo wa maisha usiofaa.

Amesema kwa kawaida wazazi na walezi wanatakiwa kuwa kielelezo kwenye familia zao kwa kuweka utaratibu wa kukaa na watoto wao na kuwafundisha  maadili ya dini naya kijamii ilikuwajaza imani ma siyo kuwaachia makukumu yote wadada wa kazi kwani majukumu ya kumuandaa makuzi ya mtoto yanatakiwa kufanywa na wazazi wenyewe.

Mchungaji Mtashi amkesema ni vema wazazi kuona umuhimu wa kukaa na watoto wao na kuwapa maadili ya dini na kuwafundisha imani  ili waweze kuwa na maamuzi yenye tija kwa baadaye na kusaidia kupunguza ama kuondoa watoto wanaongeuka kitabia na kiakili wanapokuwa wakubwa kiasi cha kushinwa kuwatunza wazazi.

Ameongeza kuwa inasikitisha kuona wazazi wanakuwa wavuvi wa kulea watoto wao na kuwaachi wadada wa kazi kitu ambacho kinaashiria uvuvi wa kulea na kutekeleza majukumu yao kwa watoto wakiwa kama wazazi.

Amesema imani  inakuja kwa kusikia neno la kristo hivyo ni lazima wazazi kuona umuhimu wa kuwafundisha  watoto wao ili waweze kuwa watii wa familia zao kwani watoto hutoka  mikononi mwa wazazi wao pindi wanapomaliza masomo yao na baadae kujitegemea na kufanya maamuzi.

“Waefeso 6:1-4 maandiko yanasema enyi watoto watiini wazazi wenu katika bwana maana hii ndiyo haki, waheshimu baba na mama yako kwani amri hii ni ya kwanza yenye ahadi ili mpate heri na ukae siku nyingi  katika dunia, nanyi msiwachokoze watoto wenu bali waleeni katika adabu na maonyo,” amesema Mtashi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,220FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles