29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, September 18, 2021

Wazazi wapewa somo la barakoa

Na Renatha Kipaka, Bukoba

WAZAZI wa manispaa ya Bukoba, wametakiwa kutoa ushirikiano wa kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule wakiwa wamevaa barakoa safi  ili kujikinga na maambukizi ya Corona.

Ombi hilo limetolewa na mkuu wa shule ya Msingi Quidus,​ iliyopo Bukoba, Elias Kateme, wakati mwandishi wa Mtanzania Digital, alipofika kwenye shule hiyo kujionea jinsi wanafunzi wanavyojikinga na Covid-19.

Kateme amesema,endapo wazazi wakitoa ushirikiano itasaidia watoto kuwa salama  katika maeneo yote, nyumbani na shuleni.

“Wazazi wenzangu tujitahidi kuwanunulia watoto barakoa hasa wakiwa shuleni, sehemu ambayo ina mkusanyiko mkubwa ili wawe salama hiyo itawaweka vizuri tofauti na wale ambao hawavai,”amesema Kateme.

Ameeleza kuwa katika shule ya Qudus, wamewekwa miundombinu ya maji tiririka karibu na milango ya kuingilia darasani pamoja na milango ya utawala na katika milango ya vyoo vya wanafunzi.

“Sisi katika kuzingatia elimu inayotolewa na Serikali yetu tumeweka utaratibu wa mwanafunzi anapotoka na kuingia ananawa mikono bila kujali anatoka wapi,” amesema Kateme

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,718FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles