NA MWANDISHI WETU, KIBAHA
WAZAZI, walimu na walezi wametakiwa kuwajenga watoto ili watambue hakuna mbadala wa kujituma na nidhamu hata kama wamezaliwa katika familia yenye kila kitu.
Hayo yamebainishwa leo na Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dk, Indiael Kaaya akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya tano ya New Version Nursery & Primary School iliyopo Kibaha.
“Natamani watoto wajue hakuna mbadala wa kujituma na kuwa na nidhamu kwa sababu kila aliyefanikiwa katika maisha kuna wakati alijituma na kujinyima hivyo ukipata nafasi ya kufanya kitu iwe shule ama ofisini fanywa kwa ufanisi na bidii yako yote na nidhamu ya kujua unachotaka kukifanya ukifanye kwa wakati gani,” amesema Dk Kaaya.
Amewata wazazi, walimu kuwasaidia watoto kutumia vipaji vyao kwa sababu watu wengi waliofanikiwa na kufikia malengo yao ni wale ambao wanachanganya elimu waliyonayo na vipaji vyao.
“Ukiona mtoto wako anapenda kufanya kitu Fulani ikiwemo kupika mpe fursa na utengenezee mazingara ambayo yatamfanya alipate madhara.
Dk Indiael amewataka wazazi kujitahidi kuwawekea watoto mipaka ya simu, na siyo watoto tu hata watu wazima kwa sababu wakimezwa na simu ni lazima wapoteze ufanisi katika shughuli zao za kila siku na kuleta madhara.
Kwa upande wa Mkuu wa Shule hiyo, Zulfa Lema amesema shule hiyo imekuwa ikifanya mitihani ya kitaifa na kushika nafasi tatu bora wilaya na mkoa wa Pwani na mwaka 2017 ilifanikiwa kushika nafasi ya 96 kitaifa na mwaka jana ilishika nafasi ya 175 kitaifa.
Malengo tuliyojiwekea tangu shule kuanzishwa yao si kufaulisha watoto tu bali kuhakikisha vijana wetu wanapata nafasi katika shule za watoto wenye vipaji maalum jambo ambalo limekuwa likitokea mwaka hadi mwaka. Ni maombi yetu hata vijana wetu waliomaliza eli yao ya msingi mwaka huu nao wapate nafasi hizo adhimu.