27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi wakamatwa kwa kuozesha binti wa miaka 14

NA ALLAN VICENT-Nzega

JESHI la Polisi wilayani Nzega mkoani Tabora kwa kushirikiana na Shirika la Kupinga Ndoa za Utotoni (VSO) la mkoani Shinyanga, wamefanikiwa kuzuia sherehe ya ndoa ya kuolewa binti wa miaka 14 iliyokuwa ikifanyika kijiji cha Kipilimka wilayani hapa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo, Robert Mwanga alisema tukio hilo limetokea hivi karibuni katika kijiji hicho ambapo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, wahusika wote wakiwemo wazazi, maharusi na mshereheshaji wa harusi hiyo walikamatwa na polisi.

Alilishukuru Shirika la VSO kwa juhudi zake za kuelimisha jamii umuhimu wa kutoa taarifa punde waonapo wazazi au walezi, wakipanga kuozesha watoto wa kike walio na umri chini ya miaka 18, elimu ndiyo imesaidia kusambatishwa kwa ndoa hiyo.

Alisema shirika hilo, baada ya kupata taarifa za mipango ya ndoa hiyo walitoa taarifa kwa maofisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Nzega na Shinyanga kwa kuwa muolewaji alikuwa na makazi ya pande mbili,.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga, Deus Mhoja alisema baada ya kupata taarifa za binti wa miaka 14 aliyetoroka kutoka Nzega na kuja mkoani humo na wazazi wake wanapanga kumwozesha aliwasiliana na mwenzake wa Nzega na kuweka mtego uliofanikisha kukamatwa wahusika mwakilishi wa VSO, Aden Zahend alisema  taarifa ya uwepo wa ndoa waliipata kutoka kwa wasamaria wema ambao walipata elimu ya mapambano dhidi ya ndoa za utotoni mkoani shinyanga. 

Alitoa wito kwa jamii kuendelea kupinga vitendo, vinawadhalilisha watoto wa kike walio na umri mdogo na kuwanyima fursa za kupata elimu ili waweze kutimiza ndoto, aliahidi mapambano dhidi ya vitendo hivyo yanaendelea.

Aliongeza  hadi sasa wazazi wa pande zote mbili wanaendelea kushikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles