27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi waiangukia Serikali kesi za mimba

 ALLAN VICENT

BAADHI ya wazazi na walezi wilayani Kaliua mkoani Tabora, wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaokwamisha kwa makusudi au kumaliza kinyemela kesi za watu wanaotuhumiwa kuwapa mimba watoto wa shule.

Wakizungumza na gazeti hili juzi, wakati wa hafla ya kukabidhiwa mifuko 100 ya saruji na mabati 40 vilivyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Ukumbi-Kakoko wilayani humo, walilalamika baadhi ya watoto wanakatishwa masomo kwa kupewa mimba au kuozeshwa.

Mkazi wa Ukumbi-Kakoko, Hemed Mkalima alisema wamekuwa wakishiriki shughuli mbalimbali za maendeleo katika kijiji chao ikiwemo kuchangia suala la elimu, wanasikitishwa na tabia ya baadhi ya watu wanaowapa mimba watoto wao kutochukuliwa hatua.

Alisema baadhi ya wahusika wakikamatwa na kupelekwa katika vyombo vya sheria, kesi zao zimekuwa zikishindwa kuendelea au kwisha kinyemela wakati watoto wao wanaopata mimba au kuozeshwa wakishindwa kuendelea na masomo.

Alibainisha baadhi ya watumishi wa serikali, wazazi na walezi wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kesi za mimba, ndoa na ubakaji watoto kushindwa kuendelea katika vyombo vya sheria kwa kuzimaliza kinyemela ili kulinda wahusika.

Ramadhani Maganga, alielezea kusikitishwa kwake na matukio ya wasichana kupewa mimba au kuozeshwa katika umri mdogo hivyo kukatisha masomo yao mapema, huku wengine wakipata matatizo wakati wa kujifungua. 

‘Tunaomba hatua kali za kisheria zichuliwe kwa wale wote watakaobainika kukatisha masomo watoto wetu wa kike kwa kuwapa mimba au kuwaoa, na wale wote watakaokwamisha kesi hizo au kuzimaliza kinyemela wawajibishwe’, alisema.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Abel Busalama alisema takribani asilimia 30 ya watoto wakiwemo wa kike wamekuwa wakishindwa kuhitimu elimu ya msingi na sekondari kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo mimba na ndoa za utotoni na wote wanaobainika wamekuwa wakichukuiwa hatua stahiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Dk.John Pima aliwataka wananchi kutoa taarifa za matukio ya namna hiyo ili wahusika wote wakamatwe na kufikishwa mahakamano haraka.ikiwemo watumishi, wazazi na walezi wanaolinda watuhumiwa.

Meneja-Ukarabati Miundombinu wa TRC, Mhandisi Machibya Masanja alisema wametoa msaada huo ili kuimarisha ujirani na ushirikiano mwema na wananchi wa kijiji hicho kwa kuwa wametoa mchango mkubwa kufanikisha ukarabati wa miundombinu ya reli iliyosombwa na maji. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles