24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAZAZI WAASWA MALEZI YA WATOTO

DAR ES SALAAM


WAZAZI wametakiwa kushirikiana na walimu katika malezi ya watoto  kuwawezesha kukua katika maadili mazuri.

Hayo yalizungumzwa mwishoni mwa wiki   Dar es Salaam na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Loyola, Daud Kalimi.

Alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kuwaaga wahitimu wa darasa la saba na chekechea katika Shule ya Msingi Kilimani  Mbezi Juu.

Alisema wazazi nao wanatakiwa kuwasoma  watoto wao wanapokuwa wanasoma  kuwasaidia katika masomo au  nidhamu ambayo itawasaidia kufikia malengo yao katika maisha ya baadaye.

Alisema wazazi wanatakiwa kushirikiana na walimu kuwalinda watoto  kuwaepusha na watu ambao wanaweza kuwafundisha mambo ambayo ni tofauti na maadili.

“Kwa wale watoto wanaosoma shule za kutwa anapotoka nyumbani kabla hajafika shule au hajafika nyumbani baada ya kutoka shule hapo njiani anakutana na mwalimu mwingine ambaye hatuwezi kujua anamfundisha nini hasa ukizingatia hali ya sasa wazazi wengu tumebanwa na majukumu hivyo muda wa kuwafuatilia watoto ni mdogo,” alisema Kalimi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Kilimani, Mkomwa Mtiga alisema   shule ya Loyola imekuwa na mchango mkubwa katika shule ya Kilimani,

Alisaema hiyo ni kwa sababu  inatoa ufadhili kwa wanafunzi wa shule hiyo ambao hukosa fursa za kuendelea na masomo ya sekondari ikiwa ni pamoja na kuwajenga katika maadili.

Alisema mchango wa elimu ni mkubwa na kwamba kuelekea serikali ya viwanda haiwezekani kupata wahandisi wazuri bila kuwekeza katika elimu.

“Natoa wito kwa wazazi na serikali kuwekeza katika elimu kuanzia shule ya awali, msingi, sekondari na kuendelea  kuweza kufikia malengo yetu ya serikali ya viwanda,” alisema Mtiga.

Mwalimu Francis Njoroge ambaye ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, alisema kuwa elimu ni sekta muhimu ambayo wawekezaji wanatakiwa kuwekeza  kuisaidia jamii  na kujenga kizazi kinachojiamini.

Alisema walimu pekee hawawezi kuwafuatilia watoto katika kuwajenga katika maadili na kwamba wazazi wanatakiwa kuwasaidia  kuwawezesha kufanya vizuri katika masomo yao  na maisha yao ya baadaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles