27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi Msoma Vijiji wamshukuru Prof. Mhongo

Na Shomari Binda, Musoma

WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Sekondari Tegeruka iliyopo jimbo la Musoma vijijini, mkoani Marawamemshukuru Profesa Sospeter Muhongo, kwa kukubali kushirikiana nao ili kufanikisha ujenzi wa maabara na maktaba shuleni hapo.

Kauli ya wazazi hao imekuja siku chache baada ya mbunge wa Musoma vijijini, Profesa Muhongo, alipotembelea shule hiyo kuangalia maendeleo ya usajili wa muhula mpya wa masomo.

Mmoja wa wananchi hao, Mariam Masatu, mkazi wa Kijiji cha Tegeruka, amesema watashirikiana na mbunge ili kuweza kutimiza ujenzi huo.

Amesema Profesa Muhongo amekuwa akiahidi na kutekeleza hivyo wanaamini katika ujenzi wa maabara na maktaba ya shule ya sekondari Tegeruka atafanya hivyo pia.

Mariam amesema elimu ni suala la muhimu na mbunge amekuwa akifanya jitihada kubwa kwenye eneo hilo na wao kama wananchi watamuunga mkono kwa kuweka nguvu na kufanikisha kila hitaji muhimu.

“Juzi mbunge wetu ametembelea shule ya Tegeruka na kukubali kuchangia ujenzi wa maabara na maktaba, nasisi tutamuunga mkono. Tunamuamini mheshimiwa Muhongo kwenye kuchangia miundombinu ya elimu kwenye jimbo letu na leo kuna mabadiliko makubwa,” amesema Mariam.

Kwa upande wake mkazi wa Kijiji cha Mayani, Juma Musa, amesema maabara na maktaba ni jambo muhimu hasa kwenye masomo ya Sayansi, hivyo ni muhimu kumuunga mkono mbunge huyo.

Profesa Muhongo amekuwa akishirikiana na wananchi katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya elimu jimboni humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles