23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi msilee watoto kama mayai- Machali

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Moses Machali amewataka wazazi na walezi kuwaadhibu watoto pindi wanapokosea ili kuondoa dhana ya watoto kukaa kama mayai na mwisho wa siku kulihalibu taifa la kesho.

Sehemu ya wahitimu wa kidato cha sita.

Machali ametoa kauli hiyo wakati wa mahafari ya sita ya kidato cha sita ya shule za Sekondari za Kaizirege na Kemebos katika Manispaa ya Bukoba.

Amesema kuwa watoto wanapokosea wanapaswa kuadhibiwa kwa viboko au kwa kutumia adhabu nyingine ambayo inamstahili mtoto na sio kupiga hadi kuuwa au kumsababishia maumivu makali.

“Wazazi wanapaswa kuruhusu hata shuleni watoto waadhibiwe, maana wengine mtoto akiadhibiwa shuleni wanalalamikia walimu bila kujiuliza athari zake, lakini hizo adhabu zisiende kinyume na mwongozo na sheria,” amesema Machali.

Machali ameongeza kuwa amefanya utafiti na kujua kwamba shule za Kaizirege na Kemebo zinatoa adhabu ya viboko kwa watoto ili kuwafundisha kuwa wakifanya vibaya watapokea tuzo hasi.

“Acheni kuwalea watoto kama kuku wa kisasa, wazazi wenzangu naomba mnielewe, tukifanya hivyo tunawapumbaza watoto wetu, tunawafanya wa kudekadeka tuna haribu nguvu kazi ya taifa, amesema Machali.

Naye Meneja wa shule za Kemebos na Kaizirege, Eulogius Katiti amewataka wahitimu wa kidato cha sita kuzingatia masomo watakapokwenda nyumbani kwa muda watakao kuwa wakisubiria kwenda kuendelea na elimu ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles