28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wazalishaji kutoagiza sukari 2022/2023 kulipandisha bei ya bidhaa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kitendo cha kampuni za wazalishaji kutoagiza sukari nje ya nchi katika msimu wa 2022/2023, kulisababisha bei ya sukari kupanda na kuongeza hali mbaya ya upatikanaji wa sukari nchini.

Hayo yamesemwa leo Julai 5,2024 na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya baadhi ya wadau wa sukari kuzungumzia Sakata hilo licha ya kukosa taarifa za kutosha.

“Kampuni nne zilipewa vibali lakini ni kampuni moja tu ya Kilombero kati ya nne iliingiza sukari tani 2,380 licha ya wazalishaji kupewa vibali vya kuagiza sukari kwa msimu huo. Kitendo cha wazalishaji kutoingiza kiasi chote cha sukari kilichoidhinishwa 2022/23 kilisababisha upungufu na kupanda bei hadi kufikia shilingi 4,000 kwa kilo moja mwezi Juni, 2023,” Alisema Profesa Bengesi.

Katika hatua nyingine, Profesa Bengesi alisema kitendo cha kushindwa kwa wazalishaji kuingiza sukari katika msimu wa 2022/2023 kuliwapotezea sifa ya kisheria ya kupewa vibali kwa msimu wa 2023/2024, lakini bado serikali iliendelea kuwapa vibali vya kuendelea na shughuli ya uingizaji wa sukari nchini Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles