25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAZABUNI ILIBORU WATOA SIKU 14 WALIPWE MADENI

Na ELIYA MBONEA

-ARUSHA

WAZABUNI wa chakula katika Shule ya Sekondari ya wanafunzi  wenye vipaji maalum ya Iliboru ya jijini hapa, wametoa   siku 14 kulipwa madeni yao zaidi ya Sh milioni 690.

Vilevile wametishia kurejesha kesi mahakamani baada ya siku hizo kupita bila kulipwa madeni yao  baada ya kutoa huduma ya chakula katika shule hiyo tangu mwaka 2015.

Walilazimika kusimamisha  kutoa chakula kutokana na kufilisika.

Wakili wa wazabuni hao, Shahibu Mruma, alisema  walikabidhi kusudio la kuifikisha mahakamani shule hiyo baada ya awamu ya kwanza ya uongozi wa shule hiyo ambao uiomba shauri hilo lisiendelee mahakamani  uweze kufanya mchakato wa malipo.

“Zaidi ya miezi mitatu iliyopita tuliwapa notisi hiyo lakini uongozi wa shule na serikali waliomba kupewa muda wa kulipa.

“Ia mpaka sasa ni zaidi ya miezi sita hawajalipa, tunawapa siku 14 wasipolipa tutarudi mahakamani,” alisema Wakili Mruma.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Big Expedition, Nicolaus Minja alisema watarejesha suala hilo katika vyombo vya sheria iwapo muda huo utapita bila hatua yoyote ya malipo kufanyika.

Alidai   awali aliyekuwa Mkuu wa Shule hiyo, Julius Shulla, baada ya kupokea notisi ya kwanza ya kutaka kufikishwa mahakamani  Januari mwaka huu, aliomba kupewa muda wa kufanya mchakato wa malipo kutokana na   uhakiki wa deni hilo kuendelea lakini mpaka sasa bado hawajalipwa.

Alisema   baada ya kuombwa kusubiri uhakiki ufanyike, waliendelea kusubiri ambako viongozi mbalimbali akiwamo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ambao walieleza kuhusu tatizo hilo baada ya kupokea malalamiko ya wazabunu hao,   waliahidi kuwa watalipwa.

Aliyekuwa Mkuu wa Shule hiyo ambaye amehamishiwa mkoani Morogoro, Julius Shulla, alikiri kuwapo   madai ya wazabuni na kueleza uongozi wa shule hiyo  ulikuwa haujapokea malipo hayo.

Wazabuni wengine wanaodai shule hiyo ni   Domica Mosha, Laurice Tarimo na Elipendeza Richard ambao wote tayari walifikisha madai yao  kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Serikali (CAG) na kuahidiwa wangelipwa baada ya kukamilika uhakiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles