24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wawili wauawa kwa kipigo cha wananchi

Damian Masyenene – Shinyanga

WATU wawili ambao majina, umri na makazi yao hayajafahamika wamefariki dunia baada ya kushushiwa kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira mjini Kahama wakiwatuhumiwa kuiba runinga na redio ya kisasa.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba, ilieleza kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 19, mwaka huu saa 7 mchana katika Mtaa wa Majengo mjini Kahama.

Alisema kuwa marehemu hao ni waname wenye umri kati ya miaka 20-25  walikutwa na umauti kutokana na hali yao kuwa mbaya kutokana na kujeruhiwa kwa kurushiwa mawe sehemu mbalimbali za miili yao na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kuwakuta njiani wakiwa wameiba Televisheni (Flat Screen) aina ya Tandar na Subwoofer zenye thamani ya jumla Sh 345,000 mali ya Ayoub Kigi mkazi wa Majengo.

“Majeruhi walikimbizwa hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa ajili ya matibabu kutokana na hali zao kuwa mbaya, lakini walifariki wakiwa wanaendelea na matibabu hospitalini hapo….chanzo cha tukio hilo ni wananchi kujichukulia sheria mkononi baada ya kuwatuhumu vijana hao kuwa ni wezi, juhudi za kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa waliohusika na tukio hilo zinaendelea,” alisema Kamanda huyo.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wanne akiwemo mwanamke mwenye umri wa miaka 57 wakiwa na dawa za kulevya aina ya Heroine pinchi nane.

Waliwataja watuhumiwa wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo la kukutwa na dawa za kulevya kuwa ni Hassan Ibrahim (22), Juma Omary (26), Abdalah Hemed (23) na Chiku Tungu (57) ambao walinaswa Aprili 19, mwaka huu saa 6 mchana katika Mtaa wa Majengo Mjini Shinyanga baada ya askari kupata taarifa za kiintelejensia na kufika nyumbani kwa mtuhumiwa Chiku Tungu.

Alisema baada ya kuwakamata watuhumiwa hao ambao walikuwa ndani ya uzio wa nyumba hiyo na dawa hizo za kulevya wakiwa na rizla, kitezo, kigae na kisu kimoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles