29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

WAWILI WAFARIKI IRINGA KWA KUJINYONGA


Na FRANCIS GODWIN-IRINGA   |  

WATU wawili wamefariki dunia kwa kujinyonga mkoani Iringa, akiwamo raia wa India aliyejinyonga baada ya mkewe kwenda kwao India bila ridhaa yake.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Juma Bwire, alitoa taarifa hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Kamanda Bwire, matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti katika Kijiji cha  Tagamenda, Kata ya Luota, Wilaya ya Iringa Vijijini.

“Mkazi wa kijiji hicho, Waziri Nzengere (43) ambaye ni mkulima, alikutwa akiwa amejinyonga shambani kwake kwa kutumia kamba.

“Kwa hiyo baada ya uchunguzi wetu kukamilika uliohusisha madaktari, ulionyesha kifo hicho kilitokana na kujinyonga na mwili wa marehemu umeshakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi,” alisema Kamanda Bwire.

“Katika tukio la pili, Machi 26, mwaka huu, majira ya mchana, polisi walipewa taarifa za kifo cha Hiren Shantilal Makvana (29), mwenye asili ya India aliyekuwa akifanya kazi katika ofisi ya electronic techical- Aitel Iringa akiishi eneo la Gangilonga mjini hapa, baada ya kukutwa amejinyonga.

“Katika tukio hilo, Hiren alikutwa amejinyonga katika  chumba chake alichopanga kwenye jengo la NSSF, Kata ya Gangilonga.

“Marehemu alikuwa amejifunga nguo shingoni na kisha kuifunga katika feni iliyokuwa ndani ya chumba chake.

“Pamoja na kifo hicho, inaonekana mke wa marehemu huyo alikuwa amesafiri siku za nyuma kwenda nchini India katika mazingira ambayo hatujayajua vizuri.

“Lakini pia, marehemu hakuacha ujumbe wowote juu ya tukio hilo na sasa tunaendelea na upelelezi ili kujua chanzo cha tukio hilo,” alisema Kamanda Bwire.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,220FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles