Wawili jela miaka 20 kwa kuingia hifadhini

0
498

NA, MALIMA LUBASHA

WAKAZI wa Kijiji cha Machochwe Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Mugaya Bisara(54)  na Andrea Chacha (20),wamehukumiwa kwenda jela miaka 20 kila mmoja na Mahakama ya Wilaya ya  Serengeti, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti bila kibali.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti,Ismael Ngaile alisema washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kuingia ndani ya hifadhi,kupatikana na silaha na nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Alisema mahakama imetoa adhabu hiyo, baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka bila kuacha shaka yoyote.

Akitoa hukumu hiyo,Hakimu Ngaile alisema katika kosa la kwanza la kuingia ndani ya hifadhini,washtakiwa mbali na kukana makosa walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu,kosa la pili la kuingia na silaha walihukumiwa kifungo cha miaka miwili na kosa la tatu la kupatikana na nyara za Serikali, walihukumiwa miaka 20.

Hakimu Ngaile,alisema mbali na Serikali,viongozi wa vijiji kutoa elimu ya uhifadhi wanyamapori nakuwataka kuwa walinzi wa rasilimali hiyo kwa faida ya Taifa,jamii bado haizingatii maelekezo na maonyo mbalimbali yanayotolewa.

Awali waendesha mashtaka, Renatus Zakeo wa Polisi akishirikiana  na wale  Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA),  Emmanuel Zumba,akisoma hati ya mashtaka  namba 78/2018, ilidaiwa Agosti 6, mwaka jana saa 12.00 jioni eneo Machochwe ndani ya Hifadhi ya Serengeti walikamatwa wakiwa na silaha na nyara bila kibali.

Waendesha mashtaka hao, waliomba mahakama kutoa adhabu kali ili liwe fundisho kwa watu wengine na onyo kwa watu wanaoingia ndani ya hifadhi  na mapori ya akiba kufanya vitendo vya ujangili huku waki jua kuwa ni kosa.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here