Elizabeth Kilindi,Njombe
Wawekezaji nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji wa zao la kilimo cha parachichi yanda za juu kusini ili kupamba na tatizo la lishe bora kwa jamii.
Ushauri huo umetolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani na Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Nyanda za juu Kusini, Venance Mashiba, ambapo amesema wamekua wakitoa elimu juu ya fursa za uwekezaji zilizopo nchini ikiwemo kilimo hicho.
“Katika maonyesho haya sisi kama wadau tukijaribu kutoa elimu kuhusiana na fursa za uwekezaji katika nchi yetu,fursa ambazo katika nchi yetu,fursa ambazo kwa nanmna moja au njengine zinaweza kuboresha lishe ya watanzania lakini kuboresha lishe kwa ujumla.
“Katika upande wa kilimo na chakula, Nyanda za Juu Kusini kuna zao la parachichi ambalo kwa sasa hivi ni zao la kimkakati katika eneo letu hili la mkoa wa Njombe kwa hiyo na sisi tuko hapa baada ya kufanya tafiti mbalimbali na kupata mnyororo wa thamani kubwa zaidi uliopo kwenye zao la parachichi. Tumeona ni vyema taarifa hizi tukazileta kwa wananchi ili kuwaelekeza katika parachichi sio kilimo cha parachichi tu kuna vitu vyengine unaweza ukavifanya na ukawa ni muwekezaji katika mnyororo wa zao la parachichi,” alisema Mashiba.
Hata hivyo alisema kuwa kwa upande wa ufugaji kuna tafiti zimefanyika kuhusiana na mifugo mbalimbali ambayo ni mnyororo mzima wa uongezaji thamani katika mazao ya mifugo.
“La tatu ni upande wa uvuvi ambapo tumeleta fursa zilizopo katika ufugaji wa samaki haya zote ni sehemu ya maadhimisho haya kwa sababu kutokana na fursa zilizopo katika maeneo haya zinaweza zikasaidia katika kuboresha lishe kwa ajili ya wananchi,” alisema Meneja huyo.