31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Wawakilishi wa walemavu watoke miongoni mwao’

zitto10 JOHANES RESPICHIUS

-Dar es Salaam

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameshauri wabunge ambao wanawakilisha watu wenye ulemavu watokane na kundi la walemavu husika.

Zitto aliyasema hayo jana wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya viziwi kimataifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

Alisema utaratibu wa wabunge hao kutoka ndani ya vyama vya siasa unapunguza uwakilishi wa makundi hayo bungeni.

“Katika mfumo wa siasa tuweke nafasi za wabunge wenye ulemavu kupaza sauti kwa niaba ya wenzao lakini mfumo huo haupo kwenye mabaraza ya madiwani ambako matatizo mengi yanapatikana kule.

“Lakini licha ya kuwa na uwakilishi huo bado hawajawakilishwa sawa sawa kwenye wabunge hao wanatokana na vyama vya siasa ambapo ikitokea hoja hata kama ni mbaya kwa watu wenye ulemavu hawezi kuipinga kwa sababu anafurahisha chama chake.

“Hivyo basi tunahitaji maboresho ya sheria ili wawakilishi wa watu wenye ulemavu wachaguliwe na walemavu wenyewe tofauti na mfumo uliopo sasa,” alisema Kabwe.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) alizishauri taasisi za benki kuweka mfumo wa kutoa mikopo isiyokuwa na masharti magumu kwa watu wenye ulemavu tofauti na ilivyo sasa.

Naye Mwenyekiti wa Furaha ya Wanawake Viziwi Tanzania (FUWAVITA), Aneth Gerana, alizikaribisha taasisi mbalimbali ambazo zinataka kuwekeza kwenye vikundi vyao.

“Tunaomba wadau watuunge mkono katika shughuli zetu ambazo tunazifanya maana ujuzi na ubunifu tunao labda kinachokosekana ni rasilimali fedha tu.

“Katika jitihada zetu za kuwekeza tumepata eneo la kujenga kiwanda lakini hatuna fedha hivyo tunaomba tuunganishwe na wawekezaji ili azma yetu iweze kutimia ya kuwa na kiwanda chetu kama njia ya kutimiza lengo la Serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa viwanda,” alisema Aneth.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles