26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Wawa kuikosa TP Mazembe

TIMA SIKILO

BEKI wa kati wa Simba, Pascal Wawa, amesema hana uhakika wa kusafiri na timu kuelekea nchini Kongo kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya TP Mazembe.

Wawa ameumia kifundo cha mguu wiki iliyopita wakati akiwa anajaribu kuokoa mpira katika mchezo wa kwanza wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Aprili 6.

Akizungumza na Mtanzania Digital Wawa amesema kutokana na maumivu aliyoyapata kwenye mchezo huo anakuwa njee ya uwanja kwa muda wa wiki moja au mbili.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri nimekwenda hospitali, nimeshafanyiwa vipimo, sidhani kama nitakuwa miongoni mwa kikosi kitakachosafari kuelekea nchini Kongo.

“Nimepata majeraha, yanaweza kuniweka nje kwa muda wa wiki moja au mbili,” amesema Wawa.

Katika mchezo huo Wawa aliomba kutolewa dakika ya tatu ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Juuko Murushid.

Aidha Wawa amewatuliza mashabiki wa Simba kwa kuwataka watambue kuwa hakuna kitakacho haribika katika mchezo wa marudiano. Ameongeza kwamba upo uwezekano wa yeye kaanza kucheza mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,631FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles