25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

WAUZA DAWA ZA KULEVYA WABADILI MBINU KENYA

NAIROBI, KENYA


WAFANYABIASHARA wa dawa za kulevya wamebadili mbinu ya kuuza na kusambaza baada ya Serikali kuivalia njuga biashara hiyo haramu.

Baada ya Serikali kufunga mianya ambayo wafanyabiashara hao walikuwa wakiitumia kusafirisha bidhaa zao, hususan mipakani, ufukweni, bandarini na hata uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi mjini Mombasa, sasa wanatumia njia za mtandao kuendeleza biashara zao.

Kwa mujibu wa mwanaharkati wa dawa za kulevya kutoka Kituo cha Reachout, Taib Abdulrahman, wafanyabiashara hao sasa wanatumia njia za mitandao kuendeleza biashara hizo ili kukwepa kukamatwa.

Alisema wafanyabiashara hupokea pesa kwa njia ya simu ili kutojulikana wanavyoendesha biashara yao.

Abdulrahman alisema licha ya vita dhidi ya mihadarati kupamba moto eneo la Pwani, watumiaji sugu wa mihadarati wako hoi bila ya msaada wa kupelekwa vituo vya kurekebisha tabia.

“Hapo awali walikuwa wanauza wazi wazi, lakini mambo yamekuwa magumu, sasa wanatumia mtandao, hii inamaanisha mzigo unapelekwa kwa mteja alafu fedha zinatumwa kupitia mtandao kama m-pesa. Ndio maana unaona ni vigumu kwa Serikali kukamata mshukiwa akiwa na fedha,” alisema Taib.

Aidha, Taib alisema maskani nyingi ambazo vijana walikuwa wanatumia dawa za kulevya zimefungwa.

Taib aliitaka Serikali kuvumbua mbinu ya kukabiliana na jinamizi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles