28.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Waumini wampiga mchungaji  wakidai mchawi

Walter  Mguluchuma – Mpanda      

KUNDI kubwa la wananchi wakiwamo waumini,  wamevamia na kushambulia kwa mawe  nyumba ya Mchungaji wa   Kanisa la Sauti ya Uzima, Nabii Elia (36) wakimtuhumu kuwa ni mshirikina.

Jina  kamili la Nabii Elia limeelezwa kuwa ni Elia Zabron Balashika raia wa Burundi ambaye amekuwa akitoa huduma ya roho zaidi ya miaka sita eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema tukio  hilo   lilitokea Mtaa wa Kazima Ringini Manispaa ya Mpanda, baada ya waumini kuvamia nyumbani kwa kiongozi huyo.

Alisema waumini  watano wametiwa mbaroni na watu kadhaa  kutokana na kujichukulia sheria mkononi.

Aliwataja waumini  waliokamatwa  kuwa ni William  Kaluzi (19) mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa , Steven Alfred (31) mkazi wa Mtaa Kazima, Nicholaus Shadrack (33)  mkazi wa Mtaa wa Kazima  na Tekla Didas (17) mkazi wa Kijiji cha Rungwa

Wengine ambao  siyo waumini wa kanisa hilo   ni  Mashaka Moshi (23) mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa na Faraja Hussein (22) mkazi wa Mtaa wa Kazima.

Kamanda Nyanda  alisema chanzo  ni imani za ushirikina baada ya taarifa kuzagaa kuwa  Nabia Elia alikuwa ameweka ‘misukule’ watano nyumbani kwake  ambao waumini   wa kanisa hilo walimtaka awatoe  hadharani.

Alisema siku ya tukio saa 11:30 jioni,  Nabii Elia alifka  Kituo cha Polisi mjini Mpanda ambako alitoa taarifa kuwa nyumba yake ilikuwa  imevamiwa na wananchi ambao walikuwa wanaharibu mali zake .

“Ndipo timu ya  polisi wakiongozwa na SSP Focus Malengo, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa  ya Jinai Mkoa wa Katavi, Abdallah Hussein  na Kaimu  Ofisa Upelelezi  Wilaya ya Mpanda, Mkaguzi Ngagala, walifika eneo la tukio na  kukuta kundi  la wananachi     wakiendelea kurusha mawe,“ alieleza.

Alisema walianza  kutuliza ghasia kwa kufyatua mabomu ya kishindo   kuwatawanya wananchi hao, huku  waumini wawili wa kanisa hilo wakijeruhiwa  kwa  kupigwa  mawe kichwani .

Waliojeruhiwa ni Mchungaji wa Kanisa hilo,  Mussa Elia (24) na mkazi wa Mtaa wa Kazima, Joseph Elia (29) ambao wanadaiwa kuwa ni ndugu zake na Nabii Elia .

Alisema mali za Nabii Elia zilizoharibiwa  ni  pamoja na vioo vinne vya madirisha ya nyumba yake, kioo cha nyuma cha gari lake  la Spacio,  huku thamani kamili  haijafamika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,085FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles