30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Wauguzi watakiwa kuchukua tahadhari zaidi ya corona

AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

WITO umetolewa kwa wauguzi nchini kujikinga na mlipiko wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) kwa kufuata miongozo iliyotolewa  ya  magonjwa ya mlipuko.

Wito huo ulitolewa jana Mei 12 na Mkurugenzi wa Uuguzi  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),Zuhura Mawona, ikiwa ni kilele cha wauguzi dunia.

Mawona akizungumza jijini Dar es Salaam, alisema wauguzi wote wanatakiwa kufuata maadili ya taaluma yao kwa  kuwahudumia wagonjwa kwa  kauli nzuri na upendo kwani kauli nzuri ni tiba namba moja.

Katika maadhimisho ya siku hiyo yenye kauli mbiu ya ‘Wauguzi; Sauti inayoongoza uuguzi kwa dunia yenye afya’, alisema “wauguzi wote wafanye kazi kwa kufata maadili lakini pia na miongozo tunayofata tuendelee kufanya kazi kwa kuwapenda wagonjwa tunaowahudumia sisi tupo kwaajili ya kuhakikisha kwamba tunalinda  na kuwahudumia wagonjwa na tuwapende wagonjwa wetu.”

Mawona alisema kwa kuzingatia asilimia kubwa ya watumishi wa sekta ya afya nchini ni wauguzi, Hospitali ya Muhimbili itaendelea kuwajengea uwezo wauguzi tarajali pamoja na wauguzi kutoka sehemu mbalimbali nchini ili kufanya huduma za kibingwa ziweze kupatikana nchini.

“Hospitali ya Taifa Muhimbili inapokea na itaendelea  kupokea wauguzi tarajali na kuwawekea mazingira mazuri ya mafunzo ili waje kuwa wanataaluma bora katika kutoa huduma kwa Watanzania.

“Pia tunaahidi kuendelea kuwajengea uwezo wauguzi na wakunga wanaokuja kupata uzoefu wa utoaji wa huduma katika vitengo vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum, kitengo cha kusafisafisha figo na vitengo vingine vinavyotoa huduma za kibingwa ili kuhakikisha wanapata uzoefu wa,” Alisema  Mawona.

Kwa upande wake Ofisa Uuguzi, Sofia Sanga, alisema  wanafanya juhudi katika kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu wauguzi hivyo amewataka jamii kuwa na mtazamo chanya.

“Tasnia ya uuguzi imeendelea kukua tofauti na zamani,  sasa wauguzi wanasoma katika ngazi mbalimbali hadi PHD lakini sisi wauguzi tunatakiwa kujenga upya taswira yetu kwa jamii, tutoe huduma kwa upendo na lugha nzuri na pia jamii tunaomba muondoe mtazamo hasi kuhusu wauguzi  kwasababu sisi tupo kuwahudumia ninyi,”alieleza Sanga..

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles