25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Wauguzi wapinga ongezeko la ada ya uanachama kwenye Baraza

Derick Milton, Simiyu

Wauguzi nchini wamepinga uamuzi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini (TNMC) wa kupandisha ada ya leseni za Uuguzi na ukunga bila ya kuwahusisha wenyewe ambao ndiyo walipaji wakidai hatua hiyo ni kuwanyonya.

Kauli ya wauguzi hao imetolewa leo na Katibu wa Chama cha wauguzi nchini (TANNA), Sebastian Luzinga wakati akisoma risala kwenye ufunguzi wa kongamano la kisayansi na mkutano mkuu wa 47 wa chama hicho leo mkoani Simiyu.

Luzinga amesema kuwa Baraza hilo limepandisha ada gizo bila ya wao kushirikishwa, ambapo awali walikuwa wakilipa sh.30,000 kwa wauguzi wenye astashahada na wale wenye stashahada, Shahada, Uzamili ilikiwa 40,000.

Amesema kuwa Baraza hilo limeongeza kutoka kiwango hicho hadi 40,000 kwa wauguzi wenye astashahada, 60,000 stashahada, 80,000 Shahada na Uzamili na Uzamivu 120,000.

“Ongezeko hili ni kubwa na linaathiri sana kipato cha wauguzi hawa ambao wanashindwa kukidhi mahitaji yao kwani hakuna uwiano na ongezeko la Mishahara na ada inayolipwa,” Amesema Luzinga.

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa kama chama hawakubaliani hata kidogo na uhamuzi huo, na wameiomba serikali hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wapewe majibu ya kupunguzwa kwa ada hiyo.

Hata hivyo Mkuu wa mkoa huo ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu aliunga mkono lalamiko la wauguzi hao na kusema kuwa ni kweli linawanyonya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles