30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wauguzi wamaliza mgomo wa miezi mitatu

HARARE, ZIMBABWE

CHAMA Kikuu cha Wauguzi nchini Zimbabwe kimetangaza kwamba kinawahamasisha wanachama wake kumaliza mgomo wao wa kulalamikia mishahara yao ambao ulianza mwezi Juni mwaka huu. 

Mgomo huo wa miezi mitatu umezilazimisha hospitali kuu za nchi hiyo kushindwa kupokea wagonjwa tena wakati huu wa janga la Covid-19.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, mfumuko wa bei nchini Zimbabwe ni zaidi ya asilimia 800, hali ambayo inakumbushia mazingira magumu ya zaidi ya muongo mmoja nyuma wakati mfumuko mkubwa mno wa bei uliposafisha akiba na marupurupu yote nchini humo.

Chama cha Wauguzi Zimbabwe (ZINA) ambacho kina zaidi ya wanachama 16,000 kiliitisha mgomo ili kumlazimisha Emmerson Mnangagwa kuwalipa wauguzi kwa sarafu ya dola ya Marekani lakini viongozi wa Zimbawe wanasema hawana uwezo huo.

Mgomo huo wa wauguzi na madaktari wakubwa umekwamisha shughuli za hospitali za umma huku wagonjwa wote wasio mahututi wakiwa hawapokewi kwenye hospitali hizo huku idadi ya akina mama walioharibu ujauzito wao ikiongezeka kutokana na kukosa huduma zinazotakiwa za kiafya.

Mkuu wa chama hicho cha wauguzi, Enoch Dongo alisema kuwa, wameamua kusitisha kwa muda mgomo huo ili kumpa nafasi Makamu wa Rais, Constantino Chiwenga kutatua mgogoro huo. Ikumbukwe kuwa mwezi uliopita wa Agosti, Chiwenga aliteuliwa kuwa waziri wa afya wa Zimbabwe.

Alisema, kila mwezi wauguzi wanalipwa dola 6,000 za Zimbabwe, sawa na Dola 73 za Kimarekani ikiwa ni pamoja na marupurupu. Hata hivyo takwimu za matumizi katika maisha ya kawaida ya Zimbabwe zinaonesha kuwa, familia ya watu watano inahitaji kwa uchache dola 15,573 za Zimbabwe ili isihesabiwe kuwa ni familia maskini. 

Waziri Chiwenga alisema, karibuni hivi serikali ya Zimbabwe itaacha kuwalipia mawaziri matibabu ya nje ya nchi na itatoa jedwali maalumu ya mapendekezo yake kwa sekta ya afya.

AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles