27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WAUGUZI NA WAKUNGA WASIO HUISHA LESENI ZAO KUCHUKULIWA HATUA.

MWANDISHI WETU-DODOMA

Wauguzi na Wakunga ambao watakuwa hawajahuhisha leseni zao ndani ya miezi sita kuchukuliwa hatua, ikiwemo kufutwa kwenye daftari la Uuguzi na Ukunga, hivyo kutoruhusiwa kutoa huduma kwenye vituo vya afya vya umma au binafsi.

Hayo yamesmwa leo na Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Bi. Agnes Mtawa kwenye kikao kazi cha kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji kazi wauguzi wakuu wa wilaya kinachoendelea jijini Dodoma.

“Nitoe rai kwa Wauguzi na Wakunga ambao hawajahuisha leseni zao ndani ya miezi sita, sheria inamtaka msajili awafute katika daftari la Uuguzi na Ukunga, na kama watafutwa hawatakuwa na sifa ya uuguzi na ukunga”. Amesema Mtawa.

Aidha, Msajili huyo amesema hadi sasa ni asilimia 75 ya wauguzi na wakunga wameshahuisha leseni zao na asilimia 25 waliobaki bado wanaendelea kuangalia kwenda kanzidata yao kwani wapo wauguzi ambao pengine wamefariki, kustaafu na wengine wamebadilisha kada ila kwa wale ambao bado bado wanatoa huduma za uuguzi na ukunga wanakumbushwa kuwa na leseni iliyo kwa mujibu wa sheria ya Uuguzi na Ukunga Namba moja ya mwaka 2010 na kwa wale watakaoshindwa kuhuisha leseni sheria inasema kwamba hawaruhusiwi kuendelea kutoa huduma ya Uuguzi na Ukunga.

“Taarifa imeshapelekwa kwa wahusika na orodha imetayarishwa kwa wale waliohuisha na wale ambao hawajahuhisha watakuwa wamejifuta wenyewe na hawatokuwa na sifa ya kuendelea kutoa huduma za afya na waajiri wao watatakiwa kuwachukulia hatua za kuwafuta kazi kwemye vituo vya umma na vile vya binafsi.

Hata hivyo Agnes Mtawa amewakumbusha Wauguzi kuzingatia maadili kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria kwani kumekuwa na malalamiko ya hapa na pale kuhusu utoaji wa huduma kwenye vituo vya afya hivyo kuwakutanisha wauguzi wakuu wa Wilaya kama viongozi na wasimamizi ni chachu katika kukumbushana taratibu na jinsi ya kusimamia miongozo na kanuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles