24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi wanane wa Serikali kortini

MWANDISHI WETU-Simiyu

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Simiyu, imewafikisha mahakamani kwa nyakati tofauti, watumishi wanane wa serikali kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu, Adili Elinipenda alisema watumishi  waliofikishwa mahakamani ni pamoja na makimu, mweka hazina wa halmashauri, mhasibu, mhandisi,daktari na watendaji wa kata.

Aliwataja watumishi, kuwa ni Ofisa Mtendaji

wa Kata ya Bunamala wilayani Bariadi, Kalimbiya Gambuna ambaye anakabiliwa na kesi nne za kuwakamata wazazi wa wanafunzi watoro na

kuwaweka mahabusu,kisha kuwatoa baada ya kuwaomba hongo.

Alisema Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mwamapalala wilayani Itilima, Anthony  Masiro alifikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kuomba hongo na kupokea Sh 200,000 kutoka kwa mkandarasi anayejenga barabara ya kiwango cha lami ya Bariadi hadi Maswa ili asichukuliwe hatua, baada ya kulipua miamba kwa kutumia baruti  katika muda ambao ni kinyume na

makubaliano.

Alimtaja pia Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ikindilo Wilaya ya Itilima,Sita Masunga kuwa anakabiliwa na kesi ya kuomba na kupokea hongo ya Sh 80,000  ili amwachie mtuhumiwa ambaye alikuwa mahabusu ya kata kwa

siku tatu bila kupelekwa mahakamani.

Pia alisema Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Nyakabindi wilayani Bariadi,Liberatha  Mhagama mwenye kesi ya  kuomba na kupokea hongo ya Sh 80,000 ili aandike hati ya kumtoa mahabusu (remove order), mshtakiwa aliyekuwa gerezani ambaye kesi yake alikuwa anaisikiliza.

Washitakiwa wote,kesi zao ziko Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Simiyu, zinaendelea kwa hatua mbalimbali za usikilizwaji.

Pia taasisi hiyo, imefungua kesi dhidi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,baada ya kuomba hongo na kutumiwa kwa njia ya simu kutoka kwa Michael Mahongu ambaye ni mzabuni aliyekuwa amepewa kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya Malampaka.

Aliwataja watumishi hao, kuwa ni Ernest Joseph Sitta ambaye ni Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Malampaka ambaye alipokea  Sh 72,000, fundi

sanifu wa Idara ya Maji, Salum Charles ambaye alipokea Sh 100,000, mhasibu, John  Deus ambaye alipokea Sh 150,00  na mweka hazina wa halmashauri hiyo, Journeygeorge Kiavula ambaye alipokea hongo ya Sh 300,000  toka kwa mzabuni huyo.

Alisema taasisi hiyo, imeokoa Sh 9,476,500  ambazo zilikuwa zimetumika kwa ajili ya  malipo mbalimbali ya serikali, bila kuzingatia taratibu za sheria za fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles