27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Watumishi Ujenzi, Uchukuzi watakiwa kumaliza miradi kwa wakati

Na Sheila Katikula, Mwanza

Watumishi katika wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii, umakini, na kwa kujituma kutekeleza majukumu yao kwa wakati ili waweze kuisaidia wizara na serikali kufikia malengo ndani ya muda uliopangwa.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Reonald Chamuriho wakati wa ufunguzi wa  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi uliofanyika jijini Mwanza.

Chamuriho alisema wizara hiyo itatekeleza miradi mikubwa ya Ujenzi ikiwemo Barabara,Madaraja,Vivuko,majengo ya Serikali pamoja na matengenezo ya Magari na mitambo hivyo ni vyema miradi hiyo itekelezwe na ikamilike kwa wakati.

Alisema juhudi zinaendelea kuimarisha ukaguzi wa ubora wa Barabara na viwanja vya ndege kwa kutumia mitambo maalumu ili kuzingatia vigezo na viwango vilivyowekwa.

Alisema ni vyema pia wahandisi na watumishi chini ya wizara hiyo wakaendelea kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali kwa kiwango kulingana na thamani ya fedha waliopewa ili nchi iweze kupiga hatua ya maendeleo hususani katika miundombinu.

Kwa upande wake  Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Fanuel Muhoza alisema wataangalia mikakati ambayo wataenda kuipanga kulingana na mgawanyo wa fedha zilizopo ili waweze kutoa maoni Kama kuna mapungufu hali itakayosaidia kufanya na kukamilisha kazi kwa wakati.

Naye Afisa Ugavi Mwandamizi na Mjumbe wa Tughe, Rehema Lungo alisema baada ya kikao  watahakikisha wanafanya maadhimio kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa  na Waziri ili waweze kufanya kazi kwa ushirikiano na  ufanisi mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles