Watumishi 184 kusimamia uchaguzi Serikali za mitaa

0
890

Mwandishi Wetu

Watumishi wa Umma 184 watasimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu kutoka kada mbalimbali wakiwamo Wakuu wa Idara ya Elimu za Msingi, Kitengo cha Sheria, Takwimu na Ufuatiliaji na Kitengo cha Uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa na Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), watumishi hao kutoka idara hizo zinazosimamiwa na Ofisi za Wakuu wa Wilaya kutoka mikoa mbalimbali nchini, wataapishwa kesho Alhamisi Septemba 12 ambapo uongozi wa mikoa utaratibu shughuli ya kuapishwa kwao.

“Kwa mujibu wa Kifungu 201A, cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 288 zikisomwa pamoja na Kanuni ya 3 na 6(6) ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi na Mitaa za Mwaka 2019 zilizotolewa kwa Tangazo la Serikali Namba 371, 171 na 374 ya mwaka 2019.

“Hivyo basi, kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019, Watmishi wa Umma 184 kuwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019,” imesema taarifa hiyo ya Jafo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here