24.8 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

WATUMIAJI WA MITANDAO WAHESHIMU HAKI ZA WATOTO

Na MWANDISHI WETU

NI jambo la kawaida kabisa kukuta picha za watoto katika mitandao ya kijamii kama facebook, Tweeter na Instagram.

Picha hizo ni za namna mbalimbali. Zipo za watoto wenye maradhi yenye kuvuta hisia ambapo wawekaji wa picha  hizo hutaka kuvuta hisia za wasomaji ili kupata umaarufu  mitandaoni. Wawekaji wa picha hizo mara nyingi huambatanisha mabandiko yao ya mtandaoni na maneno yanayosema; “kama unamjali mtoto huyu share (sambaza) au like (penda) picha hii!’’

Picha nyingine ambazo zimeshamiri kwenye mitandao ya kijamii ni zile za watoto wanaolelewa katika vituo vya kulea yatima. Mara nyingi wenye vituo au hata wale wanaotoa misaada wamekuwa na tabia ya kuwapiga picha watoto hao na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii na hata vyombo vya habari.

Wahisani wanaotoa misaada kwenye vituo hivyo nao hawabanduki vituoni hadi wawe wamepiga picha na kuzisambaza kwenye mitandao ili kuonyesha wema wao.

Ziko pia picha za watoto wakiwa watupu au wakiwa na nguo chache maungoni ambazo wakati mwingine hutumwa na wazazi au walezi wao.

Ni kweli kuwa nyingi ya picha hizi hutumwa kwa nia njema. Lakini, wasichojua watumaji ni kwamba baadhi ya picha hizi zinapowekwa kwenye mitandao ya kijamii huwa zinavunja haki za watoto na kuwadhalilisha.

Watoto kama ilivyo kwa makundi mengine ya kibinadamu, wanazo haki za zao na zinapaswa kuzingatiwa na watu wote kwenye jamii. Haki hizi zinalindwa pia na mikataba mbalimbali ya kimataifa na sheria za nchi.

Moja ya haki za watoto ni haki ya usiri na faragha. Kama ilivyo kwa watu wazima, haki ya watoto ya kupata faragha inalindwa na Katiba ya nchi.

Kwa mfano; ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inasema kila mtu (akiwamo mtoto) ana haki ya kuthaminiwa utu wake na kuwa na faragha. Haki hii inatolewa pia na Mkataba wa Kimataifa wa Haki ya Mtoto(Convention of the Rights of the Child, 1989).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles