25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WATUMIAJI FACEBOOK, WHATSAPP KUTOZWA KODI UGANDA

KAMPALA, UGANDA


RAIA wa Uganda wanaotumia mitandao ya jamii kama vile Facebook na WhatsApp, huenda wakalazimika kulipa ili waruhusiwe na Serikali kuitumia.

Hii ni baada ya Bunge kuidhinisha muswada huo tata juzi Jumatano.

Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa leo, wanaotumia mitandao ya jamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda (shilingi 100 za Tanzania) kila siku.

Raia pia watalipia kila shughuli ya kibiashara watakayoikamilisha kupitia simu zao, ambazo zitakuwa zikitozwa asilimia moja ya thamani yake.

Mwezi uliopita, Rais Yoweri Museveni, alikaririwa na vyombo vya habari akisema mitandao ya jamii inatumiwa zaidi kwa taarifa za udaku.

Lakini wanaharakati wa haki za binadamu hawakubaliani na madai yake.

“Ni sehemu tu ya majaribio ya kubana uhuru wa kujieleza,” Mwana Blogu Rosebell Kagumile aliliambia Shirika la Habari la Reuters.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, wabunge watatu walikosoa sheria hizo mpya na kuzitaja kama ‘utozaji wa kodi maradufu’.

Wabunge hao; Robert Kyaggulanyi, maarufu kama Bobi Wine (Kyaddondo Mashariki) na wenzake Joshua Anywarach na Silas Aogon, walisema kwa sababu watumiaji wa mtandao wa WhatsApp hupata huduma hiyo kupitia muda wa salio ambalo wanalipia ushuru, ushuru wa ziada utakuwa unakiuka haki.

Mbunge mwingine, Patrick Nsamba wa chama tawala, alisema ushuru huo utawaumiza zaidi masikini.

Ni rahisi kwa mbunge kusema asilimia moja ni kiasi kidogo cha kosi, lakini kwa watu wenye kipato cha chini ya dola moja kwa siku itawaumiza zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles