Gabriel Mushi, Dodoma
Serikali imesema ina mpango wa kuongeza tozo kwa watumiaji wa barabara ili kuiongezea fedha Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema hayo bungeni leo wakati akihitimisha mjadala wa wabunge waliochangia katika hotuba ya wizara hiyo.
Amesema Tarura imepewa asilimia 30 ya bajeti na Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) asilimia 70 kwa sababu Tanroads inasimamia mtandao mkubwa wa barabara kuliko Tarura.
Aidha, aliwataka wananchi kutumia sekta ya mawasiliano vizuri kwa maendeleo ya kichumi.
“Niwaombe watumia miundombinu ya mawasiliano kutumia kwa maslahi ya taifa na si uchochezi au picha chafu,” amesema Profesa Mbarawa.