29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Watuhumiwa wa makontena 40 wawekwa rumande

4c36Suleiman-KovaNA TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewakamata watumishi 40 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA) wanaotuhumiwa kula njama za kuikosesha Serikali mapato.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jeshi hilo linawashikilia watumishi 26 wa TRA na watatu wa Bandari kavu (ICD) ya Azam kwa kuhusika na upotevu wa makontena 329.

Aliwataja watumishi wengine kuwa ni 11 wa Mamlaka ya Bandari nchini wanaotuhumiwa kwa upotevu wa makontena 2,489 yaliyotolewa bandarini kinyume na utaratibu.

“Watuhumiwa wote wanahojiwa kwa tuhuma za kuwezesha ukwepaji wa kodi ulioisababishia Serikali hasara,” alisema Kova.

Alisema polisi wanamtafuta wakala wa forodha anayemiliki Kampuni ya Reginal Cargo, aliyemtaja kwa jina la Abdulkadil Khasim ambaye ndiye aliyeshughulikia utoaji wa makontena 329 bila kulipiwa kodi wala ushuru wa Serikali.

“Yeyote atakayetoa taarifa za kuwezesha kupatikana kwa mtu huyo atapewa zawadi ya Sh milioni 20, hivyo ni bora ajitokeze mwenyewe,” alisema Kova.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo linawashikilia watu wanne akiwemo meneja wa Benki ya CRDB kwa tuhuma za kuhusika na tukio la uvamizi wa Benki za CRDB na DCD matawi ya Chanika.

Kamanda Kova alisema tukio hilo lilitokea Desemba 9, mwaka huu ambako walinzi wawili wa SUMA JKT walipoteza maisha na walinzi wengine wanne wa kampuni ya ulinzi ya SGL walijeruhiwa.

Wakati huo huo Mamlaka ya Mapato nchini imekusanya Sh bilioni 10.07 kutoka kwenye kampuni 22 ambazo zilihusika na uondoshwaji wa makontena bandarini kinyume na utaratibu wa forodha hadi kufikia juzi jioni.

Akizungumzia suala hilo, Meneja Elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Diana Massawe, alisema kampuni sita zimemaliza kulipa kodi hiyo pamoja na adhabu huku 16 zikilipa sehemu tu.

“Kampuni 26 hazijalipa kodi hiyo ambapo kiasi cha Sh 4,789,924,609.69 zinadaiwa pamoja na ukadiriaji kufanyika na leo (jana) kuwa mwisho,” alisema Massawe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles