25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Watuhumiwa ugaidi wachafua hali ya hewa kortini

Watuhumiwa wa kesi ya ugaidi, akiwamo Sheikh Farid Hadi Ahmed (kushoto), wakitoka kwenye chumba cha mahakama baada ya kesi yao kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Picha na Jumanne Juma
Watuhumiwa wa kesi ya ugaidi, akiwamo Sheikh Farid Hadi Ahmed (kushoto), wakitoka kwenye chumba cha mahakama baada ya kesi yao kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Picha na Jumanne Juma

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

KIONGOZI wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), ametoa shutuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi akidai kuwa limewafanyia ukatili kwa kuwapiga, hali inayowafanya baadhi yao wajisaidie damu.

Sheikh Farid alitoa madai hayo jana, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, wakati kesi ya tuhuma za ugaidi inayowakabili ilipokuwa ikitajwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Peter Njike, alidai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi haujakamilika na wanaomba hati ya kuwachukua washtakiwa saba, akiwamo Sheikh Farid kwa ajili ya mahojiano.

Hakimu Riwa alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Hali hiyo ilisababisha washtakiwa kuomba kutoa maelezo yao.

“Mheshimiwa wametuomba kwenda kutuhoji tena, mara ya kwanza tulipohojiwa, polisi hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu, ni ushenzi na ukatili, walituhoji uchi wa mnyama na kutupiga.

“Kiongozi Mkuu wa Uamsho, Sheikh Mselem Ally Mselem, mwenye heshima, mfasiri wa Kur’ani, alinihadithia alipohojiwa walimfanya nini, tumepigwa na hatukutibiwa, magereza wamejitahidi, lakini hawana nyenzo za matibabu.

“Watu wameumizwa vibaya, mengine hayasemeki, wanajisaidia haja ndogo damu wiki moja hadi mbili, tunaomba tufanyiwe uchunguzi wa afya zetu, ipo siku mahakamani italetwa maiti.

“Tumekamatwa sababu hatutaki Muungano, hiyo ndiyo kesi ya msingi, tunawaambia ukweli katika mihadhara na watu wanatuamini, tunaomba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iletwe mahakamani tuijadili,” alidai Sheikh Farid.

Mshtakiwa wa 12, Salum Alli Salum, aliomba mahakama imwite daktari ili aweze kufanyiwa uchunguzi wa afya yake kwani ameingiliwa kijinai kwa nguvu.

“Mheshimiwa tunalazimishwa kutoa maelezo wanayoyataka wao, wanatuingilia kinyume cha maumbile, wanaingiza majiti, chupa, wengine wanavuja nyuma, kama unaweza hakimu twende faragha nikakuonyeshe.

“Askari ameniingilia kisha akaniingiza jiti mpaka likakatika, kungekuwa na sehemu ningekuonyesha, Jeshi la Polisi la kwanza kuvunja sheria, waliofanya madhila haya wanawatukanisha Watanganyika na kufanya waonekane wabaya,” alidai mshtakiwa huyo.

Baada ya washtakiwa hao kutoa malalamiko yao, mahakama iliwaahidi washtakiwa hao waende wakahojiwe na muda wote watakuwa katika mazingira salama.

Sheikh Faridi na wenzake 19 wanashtakiwa kwamba kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama ya kutenda kosa la kuingiza watu nchini kufanya ugaidi.

Shtaka la pili linawakabili washtakiwa wote, wakidaiwa kuwa katika kipindi hicho walikubaliana kumuingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.

Katika shtaka la tatu linalomkabili Sheikh Farid, anadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akijua ni kosa, alimuingiza nchini Sadick na Farah kufanya ugaidi.

Sheikh Farid pia anadaiwa kuwahifadhi Sadick na Farah, huku akijua watu hao walitenda vitendo vya kigaidi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Jamal Swalehe, Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally na Juma Juma.

Wengine ni Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro na Said Sharifu.

Wakati huohuo, kesi nyingine ya ugaidi inayomkabili Kiongozi Mkuu wa JUMIKI, Sheikh Mselem Ali Mselem na mwenzake, Abdallah Said Ali, imeahirishwa hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa kwa sababu Sheikh Mselem hakuwapo anaumwa.

- Advertisement -

Related Articles

5 COMMENTS

  1. Hakika ni wazi hakuna asiye juwa nini kosa la mashekhe hawa kosa lao ni kudai serekali tatu na Haki ya mzanzibari . Jee uko wapi uhuru wa mtanzania ikiwa jeshila police linafikia kuwafanyia unyama mkubwa kiasi hiki na kwa nini wananchi tuendelee kuipenda na kuipigia kura ccm . Mwisho wa ccm uko njiani. Watakufa vinwa wazi watafhalilika funiani na mpaka kesho mbele ya haki . Jee rais wa znz na tanganyika .wameridhika na haya.

  2. Huu ni uonevu ikiwa polisi waliwafanyia maovu hao watuhumiw;
    imekuwa kawaida ya polisi wetu kutuhumiwa kuwafanyia raia au watuhumiwa gitendo viovu tena vya kikatili na hata wengine kuuawa, sasa ndio najiuliza hivi hapa tz jeshi latu hili nilanamna gani? mbona linakosa weledi kwa kiasi kikubwa namna hii?

    Je hii ndio aina ya elimu inayotolewa na vyuo vya polisi hapa nchini?

    Je serikali haioni kuna haja ya kubadili mitaala inayotumika kufundishia polisi wetu na kutumia mitaala mipya itakayofanya askari wetu wawe na mbinu mbadala za kufanyia upelelezi bila kumpatia mateso mtuhumiwa na wakawa wamepata ukweli?

    Je ile sheria inayosema mtuhumiwa hana hatia mpaka atakapoingizwa hatiani na mahakama imefutwa?

    Kama sheria hiyo haijatutwa nikwanini polisi wanatenda vitendo viovu na hawafijlkishwi mahakamani kukabiliana na mkono wa sheria?

    Kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni, kwanini haki hiyo ya kikatiba haiheshimiwi na vyombo vya dola vinaipora bila kuchukuliwa hatua stahiki?

    Mwisho nawapa pole mliofikwa na masaibu hayo, kama sisi binadamu hatutendeani haki basi mtegemeeni mungu atakaye hukumu wote kwa haki siku ya kiama.

  3. Huo ni ushenzi, na unahitaji kulaaniwa na jeshi la police kulaaniwa, Washenzi wakubwa police hawa,wanatia hasira, huo sio ubinadamu,Sisi watanzania na wazanzibari tunajuwa munawatesa mashekhe wetu Ndugu zetu kwani wanakubalika kwa jamii, kwa vile wqnahamasisha muungano basi,hilo Ndio mkuki wa viongozi wenye kupenda madaraka.

    Mungu awalaani nyie.

  4. Huo ni ukatili wa kinyama.sababu si ugaidi.sababu ni uislamu na waislam.Allah awadhalilishe hapahapa hao Mayahudi ya Kitanzania.

  5. Ni kwa kiasi gani Binadamu anashindwa kukumbuka kuwa na yeye siku moja atakuwa chini ya ulinzi wa yule mtegemewa wa wote na Hajuwi kuwa katika hatua hiyo huyo alomfanyia ukatili duniani atakuja kutaka fidia yake mbele ya Muumba na huko hakuna fidia wala msamaha isipokuwa ni wake yeye Muumba tu na yule uliomkosea kwa hatua hii unafikiria mtu kama huyu atakusamehe siku ambayo hakuna kitakachomfaa mtu kitu wala mali yake isipokuwa ni matendo yake tu ya hapa duniani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles