26.5 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Watuhumiwa meno ya tembo wamlilia

Kulwa Mzee , Dar es salaam

MFANYABIASHARA Yusuf Ali, maarufu kama mpemba wa Magufuli na wenzake wanaotuhumiwa kukutwa na meno ya tembo wanamuomba Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kupokea hati za mali zisizo hamishika za ndugu zao ili watoke gerezani wamtafutie Sh milioni 90 zilizobakia kwenye mkataba.

Hoja hizo ziliwasilishwa jana kupitia Mahakama Mtandao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Kandide Nansua.

Washtakiwa kupitia mahakama hiyo ya mtandao waliiomba mahakama kumshauri DPP akubali kupokea hati za mali zisizohamishika za ndugu zao ili waweze kutoka nje kutafuta Sh milioni 90 zilizobaki katika mkataba wao wakiwa nje.

Hakimu Simba alisema sheria ya makubaliano ni mpya imeanza mwaka 2019 na kwamba makubaliano ni kati ya mshtakiwa na DPP na mahakama haihusiki popote.

“Mahakama itamshauri Wakili wa Serikali Mwandamizi wa Kisutu kushughulikia suala hilo limalizike kwa kuwa mahakama inafahamu mlundikano wa watu magerezani,”alisema na kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 13 kwa kutajwa.

Mbali ya Mpemba, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6 .

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, 2016 wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh milioni 392.8  bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Pia inadaiwa Oktoba 26, 2016 washtakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya meno ya tembo10 vyenye uzito wa kilo 13.85 vya thamani ya Dola za Marekani 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.

Wanadaiwa kuwa  Oktoba 27, 2016  wakiwa Tabata Kisukuru washitakiwa hao walikutwa na vipande vinne vya meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya Dola za Marekani 15,000  sawa na Sh milioni 32.7 .

Oktoba 29, 2016 walikutwa na vipande 36 vya thamani ya Sh  milioni 294.6   bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles