30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Watuhumiwa mauaji mwanaharakati wa tembo waendelea kusota rumande

 KULWA MZEE – DAR ES SALAAM 

WASHTAKIWA wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya mwanaharakati wa kupambana na mauaji ya tembo, Wayne Lotter wanaendelea kusota rumande baada ya Jamhuri kuendelea kudai kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. 

Akiiwakilisha Jamhuri Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon katika Mahakama Mtandao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine sababu upelelezi haujakamilika. 

Mahakama ilikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Aprili 30 kwa kutajwa. 

Washtakiwa katika kesi hiyo ni raia wa Burundi Habonimana Nyandwi na Nduimana Jonas maarufu Mchungaji (40) mkazi wa Kamenge Burundi,Robert Mwaipyana, Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A, Inocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Meneja wa Benki ya Backlays, Khalid Mwinyi (33) mkazi wa Mikocheni B, Rahma Almas (37) mkazi wa Mbagala B na Mohammed Maganga (61) mchimba makaburi, Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leornad Makoye, Amino Sham, Ayoub Selemani, Joseph Lukoa, Gaudence Matemu na Abuu Mkingie. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles