23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WATUHUMIWA MAUAJI KIBITI WAKAMATWA

Na MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Rufiji, ambaye pia anakaimu Wilaya ya Kibiti, Juma Njwayo,  amesema vyombo vya dola vimewakamata watu wengi wanaodaiwa kuhusika na uhalifu wa kuua watu katika maeneo mbalimbali ya wilaya hizo.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi kwa njia ya simu jana, Njwayo alisema licha ya watuhumiwa hao kukamatwa, pia vyombo vya dola vinaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo.

“Kuna watu wanaoshukiwa ambao ni wengi wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa, kuna wengine wanatafutwa na wakipatikana watahojiwa, lakini hawajakamatwa kwa maana ya kwamba imethibitika wao ni wahalifu,” alisema.

MTANZANIA Jumamosi lilipomuuliza idadi ya watuhumiwa hao, alikataa kuitaja kwa kusema yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hawezi kutoa siri.

Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi wa maeneo hayo waendelee kufanya shughuli zao, lakini kwa tahadhari.

“Watu wanalima, wanaofanya shughuli za Serikali wanafanya, lakini haya yanafanyika tunapata uthibitisho kwa mfano wa hawa watu wanne waliouawa huku Rufiji, kwa hiyo hali iko hivyo. Tunaomba watu sasa wafanye shughuli zao kwa tahadhari, wakiona mtu wasiyemjua watoe taarifa katika vyombo.

“Pia kama wanazo taarifa watuambie, sisi tunajua hawa watu wako kwenye jamii, haiwezekani mtu asiyekujua wewe aje akupige risasi jioni, lazima awe anakujua na kama hakujui basi anashirikiana na mtu anayekujua. Hivyo tunawasisitiza hawa wananchi wetu wawe na tahadhari ya kiusalama,” alisema.

Alipoulizwa amebaini nini katika matukio hayo yanayowalenga zaidi viongozi wa Serikali, alisema suala hilo ni gumu na bado haijajulikana sababu ya uhalifu huo.

“Hatujui sababu ni nini, lakini ni kweli watu wote waliopata hilo tatizo wapo askari, wapo viongozi ama ni wa serikali ya vijiji au chama tawala,” alisema.

Awali, Njwayo alikiri wazi kuwa wananchi katika maeneo hayo wanaishi kwa hofu kwa sababu matukio si ya kawaida.

“Lazima uhofu, yaani upo nyumbani kwako unakula mtu anakuja anakupiga risasi, watu nao wanasikia mlio wa risasi lazima wapate hofu, hilo ni jambo la kila mtu mwenye akili yake timamu lazima ahofie.

“Lakini sisi kwa upande wetu wa wilaya halitupendezi jambo hili, tuna hatua nyingi tunazichukua kwa kushirikiana na Serikali Kuu kupambana na jambo hili,” alisema.

Kauli ya Njwayo imekuja siku chache baada ya watu wasiofahamika kumuua Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Muyui, Iddy Kirungi, huku mtoto wake, Nurdin Kirungi, akipigwa risasi ya tumbo wilayani Kibiti.

Wauaji hao baada ya kutekeleza unyama huo walitokomea kusikojulikana, hali inayotishia usalama wa raia na mali zao, huku wengine wakilazimika kuzikimbia nyumba zao kwa hofu ya kupoteza maisha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema linaendelea kuwasaka wahalifu na kuimarisha ulinzi.

Katika toleo la jana, gazeti hili lilimkariri, Diwani wa Kata ya Mtunda, Omary Twanga (CCM), akisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 17, mwaka huu saa 1:30 usiku na Kirungi aliuawa akiwa nyumbani kwake.

Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya mauaji ya watu mbalimbali, wakiwamo askari wa Jeshi la Polisi, viongozi wa vyama na Serikali za vijiji mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa rekodi za matukio ya mauaji katika mkoa huo, ni kwamba hadi sasa zaidi ya watu 30 wameuawa.

Tukio la hivi karibuni ni lile lililotokea Mei 13, mwaka huu, ambapo Katibu wa CCM Kata ya Bungu, Wilaya ya Kibiti, Halife Mtulia, kupigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka uani.

Aprili 14, mwaka huu, askari nane waliuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika Kijiji cha Makengeni, wilayani Kibiti.

Pia Januari 19, mwaka huu, Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Nyambunda, Oswald Mrope, aliuawa baada ya kupigwa risasi mbele ya familia yake na Februari 3, mwaka huu watu wasiojulikana walivamia nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Jaribu, Bakari Msanga, wakaichoma moto, huku yeye mwenyewe akifanikiwa kuwatoroka.

Februari, mwaka huu, watu watatu, akiwamo Ofisa Upelelezi wa Wilaya (OC CID) ya Kibiti mkoani Pwani, Mrakibu wa Polisi, Peter Kubezya, waliuawa kwa risasi.

Machi Mosi, mwaka huu, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda, Said Mbwana, naye aliuawa.

Aprili 29, mwaka huu, mkazi wa Kijiji cha Mgomba Kaskazini, Kata ya Mgomba, Ikwiriri, Hamad Malinda, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. 

Mei 5, mwaka huu, Kada wa CCM Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, Amir Chanjale, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Oktoba 24, mwaka jana, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyambunda, Ally Milandu, alipigwa risasi na kufariki dunia na Novemba 6, mwaka jana, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyang’unda, Kijiji cha Nyambunda, Mohammed Thabiti, alipigwa risasi akielekea kwake.

Wengine waliouawa ni Ofisa wa Misitu aliyekuwa Mkaguzi wa Kituo cha Ukusanyaji Mapato ya Ushuru katika Kijiji cha Jaribu, Peter Kitundu na Rashid Mgamba, ambaye ni mlinzi na mgambo walipigwa risasi kichwani na begani na walifariki dunia papo hapo eneo la tukio.

Pia Katibu wa CCM Wilaya ya Kibiti, Zena Mgaya, alikaririwa na vyombo vya habari akisema Kijiji cha Nyambunda, Kata ya Bungu, kimeshapoteza mwenyekiti, mtendaji na wenyeviti watatu wa vitongoji vilivyoko katika kijiji hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles