26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

WATUHUMIWA 11,071 DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA

Na Fredy Azzah, Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, imekamata watuhumiwa 11,071 na kati yao 3,486 ni wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambao walifikishwa mahakamani.

Alisema pia katika kipindi hicho cha mwaka 2017/18, tani moja na kilo 561.28 za dawa aina ya heroin zilikamatwa kati yake kilo 196.28 zilikamatwa kwenye eneo la maji ya Tanzania na nchi kavu na tani moja na kilo 365 zilikamatwa bahari kuu.

Amesema kilo 5.2 za cocaine, tani 47.7 za bangi na tani 7.4 za mirungi zilikamatwa.

“Mamlaka pia ilikamata lita 304,513 za vimiminika vya kemikali bashirifu yabisi. Katika operesheni za utekelezaji wa mashamba ya bangi na mirungi ekari 572.75 za bangi na ekari 64.5 za Mirungi, ziliteketezwa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles