27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Watu zaidi ya 150 wauawa kwenye milipuko ya mabomu Sri Lanka

Watu zaidi ya 150 wameuawa kutokana na mfululizo wa mabomu yaliyolipuka kwenye mjini Colombo nchini Sri Lanka.

Tukio hilo limethibitishwa na Polisi ambao pia wameeleza kuwa watu wengine zaidi ya 300 wamejeruhiwa.

Mabomu matatu yalilipuka kwenye Kanisa Katoliki wakati wa sala ya Pasaka, mashambulio mengine matatu yalifanyika kwenye hoteli.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Ruwan Gunasekera, mlipuko mwingine umetokea muda mfupi katika hoteli iliyopo jimbo la kusini mwa Colombo la Dehiwala likiwa ni shambulio la saba kufanyika katika siku hii ya Jumapili.

Gunasekera amesema mlipuko wa nane umetokea kwenye kitongoji cha Orugodawatta kaskazini mwa mji mkuu.

Mpaka sasa hakuna yeyote aliyedai kuhusika na mashambulio hayo na wala idara za usalama hazijasema iwapao mashambulo hayo yalifanywa na magaidi.

Lakini kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari mashambulio hayo yalizilenga sehemu za kidini na kiuchumi.

Rais wa Sri Lanka Maithripala Sirisena amesema majeshi ya ulinzi na polisi wameshaanza uchunguzi huku viongozi mbalimbali duniani wakilaaani mashambulio hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles