29 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Watu watatu watuhumiwa kutafuna milioni 342 za mauzo ya dhahabu

ALLAN VICENT – TABORA

Viongozi watatu wa kikundi cha wachimbaji dhahabu wadogo cha Winima Group kilichopo katika mgodi wa dhababu Kitunda Wilayani Sikonge Mkoani


Tabora  wanatarajia kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kutafuna shilingi
mililioni 342 za mauzo ya kilo 1.549 za dhahabu.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani hapa leo jumatano Julai 3, kwa niaba ya wachimbaji wenzake, Shabani Seifu amesema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya wachimbaji hao kukaa kikao jumatatu Julai 1, na baadhi ya viongozi.Amesema kuwa Machi 27 mwaka huu watuhumiwa hao walikwenda wilayani Nzega kwa ajili ya kufanya mauzo ya kilo 1.5 za dhahabu zikiwa ni mali ya wanakikundi hao lakini baada ya kuuza dhahabu hiyo walirudi
wilayani Sikonge lakini hawakukabidhi mauzo hayo.Amewataja viongozi wanaotuhumiwa kuwa ni Mwenyekiti wa kikundi hichoJaphet Mbwilo, Katibu wa kikundi Godfrey Mwaniwiti na Meneja wao
Bazilio Bazilio.


Seif amedai baada ya kuuza dhahabu hiyo na kukabidhiwa kitita
chote hawakuchukua askari wa kuwasindikiza ila waliamua kununua gari
aina ya PRADO yenye namba za usajili T 294 BER kwa sh mil 10 wakati
waliafikiana kuchukua askari polisi kwa ajili ya ulinzi na posho yao
iwe sh mil 5.Wanakikundi hao walimwomba Waziri wa Madini Doto Biteko aingilie kati
ili waweze kupata haki yao pia wameliomba jeshi la polisi lisaidie
kukamatwa wahusika na kufikishwa katika vyombo vya sheria.


Naye Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa ACP Emmanuel Nley amesema kuwa wamepata taarifa za tukio hilo na uchunguzi umeanza ili kubaini ukweli uko wapi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,212FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles