22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Watu wasiojulikana waua watatu Kilimanjaro, yumo mtoto wa miaka minane

Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Watu watatu wameuwawa kikatili mkoani Kilimanjaro akiwamo mtoto wa miaka Nane kuuwawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Akithibitisha tukio hilo leo Aprili 15, Kamanda wa PolisI mkoani humo Hamis Issah amesema tukio la mtoto kukatwa mapanga lilitokea april 14 mwaka huu.

Amesema mtoto huyo akiwa amelela na mama yake watu wasiojulikana walimvamia na kumkata mapanga shingoni na mkono wa kulia.

“Mtoto Sarafina Williamu (8) ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Mavula, kabla ya kifo chake alifanyiwa tukio la udhalilishaji ambapo kesi hiyo ilitolewa hukumu,”amesema.

Katika tukio lingine mama na mtoto wake wameuwawa kwa kunyongwa hadi kufa na watu wasiojulikana.

Kamanda Issah amesema tukio hilo lilitokea April 13 mwaka huu, mama huyo Koini Molell(70) na mtoto wake Sondoo Karika(30)wamekutwa wakiwa wemnyongwa hadi kufa ambapo kijana huyo alikutwa na kamba shingoni na mama yake shingo ikiwa imelegea.

“Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi umebaini mauaji hayo yamefanywa kutokana na visasi na kwamba uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini ukweli na watuhumiwa kufikishwa kwenye vyomba vya sheria,” amesema Kamanda Issah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles