31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Watu wanane wauawa Burundi

BUNJUMBURA, BURUNDI

WATU wanane wameuawa kwa risasi kwenye mji mkuu wa Burundi, Bunjumbura usiku wa kuamkia jana.

Mji huo umekuwa ukikumbwa na mashambulizi ya risasi, milipuko ya mabomu tangu kumalizika kwa uchaguzi wa rais wenye utata miezi mitatu iliyopita.

Kwa mujibu ya walioshuhudia baadhi ya miili, ambayo ilikutwa katika barabara za vitongoji vya kaskazini mwa Bunjumbura ilikuwa na majeraha ya risasi kichwani, pamoja na alama za kamba kuashiria kuwa walifungwa nazo kabla ya kuuawa.

Afisa Mkuu wa Polisi katika eneo hilo la Mutakura, Pierre Nkurikiye amewatupia lawama wahalifu kwa maafa hayo.

Hata hivyo, inafahamika wazi kuwa mitaa ya kaskazini mwa Bujumbura ni ngome ya upinzani dhidi ya Rais Pierre Nkurunziza.

Miili sita ilipatikana katika kitongoji cha Cibitoke, ambacho kimekuwa kitovu cha maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa Rais Nkurunziza.

Makundi ya upinzani yameituhumu serikali kwa kuzindua operesheni ya ukandamizaji tangu waandamanaji waingie mitaani Mei mwaka huu kupinga muhula wa tatu wa Rais Nkurunziza waliosisitiza unavunja katiba ya taifa hilo.

Wiki iliyopita, Nkurunziza, ambaye alienda kushinda uchaguzi wenye utata wa Julai 21, alikiri kuwa mahakama imebaini kesi za maofisa wa usalama wakiua na kutesa watu.

Lakini pia baadhi ya washirika wa Nkurunziza, ambaye pia alinusurika kupinduliwa, wameuawa katika mashambulizi tofauti tofauti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles