Mecca, Saudi Arabia
Wizara ya Hija na Umrah nchini Saudi Arabia imetangaza kwa watu waliopata chanjo ya Corona ndio watakao ruhusiwa kufanya ibada ya hija mwaka huu katika Mji mtakatifu wa Mecca.
Wizara hiyo imesema watu ambao wataruhusiwa ni wale waliopata chanjo dozi mbili za Covid 19 na wale ambao wamepata chanjo dozi moja ya siku 14 kabla ya Hija na itazingatia taratibu zote za kujikinga dhidi ya maambukizi ya corona.
Saudi Arabia imeripoti kuwa na wagonjwa wa maambukizi ya virusi vya corona zaidi ya watu 393,000 na vifo vya watu Zaidi ya 6,700 vinavyotokana na virusi hivyo.
Wizara ya afya ya taifa hilo imesema watu zaidi ya milioni tano wamepata chanjo dhidi ya corona, katika taifa lenye watu zaidi ya milioni 34.
Pia mwezi uliopita mfalme Salman alifanya uteuzi wa waziri wa hija na baada ya mwezi mmoja ilifanyika Hija ndogo katika mfumo mpya wa kihistoria kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona.
Mwaka jana, waislamu 10,000 ambao ni wakazi wa Saudi Arabia ndio walipata ruhusa ya kufanya Hija takatifu ingawa mara zote huwa ni watu milioni 2.5 kutoka duniani kote na ndio wanaruhusiwa kushiriki Hija hiyo.