WATU SITA WAPOTEZA MAISHA KATIKA MLIPUKO CHINA

Yancheng, China
Watu sita wamefariki dunia katika mlipuko uliotokea kwenye kiwanda cha kemikali katika mji wa Yancheng, mashariki mwa China. 
Kwa mujibu wa viongozi wa kiwanda hicho, watu 30 pia walijeruhiwa katika mlipuko huo uliosababishwa na moto katika kiwanda hicho cha mbolea. 
Mlipuko huo umesababisha uharibifu wa mejengo lakini pia Mamlaka ya Tetemeko la Ardhi China imeripoti tetemeko la ardhi wakati wa mlipuko. 
Hata hivyo viongozi wanasema bado shughuli za uokoaji zinaendelea na taarifa kamili za tukio hilo zitaletwa hapo baadae.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here